Bonyeza Hapa ili Kusanidi Sliverlight*
KiswahiliBadili|Wavuti Zote za Microsoft
Microsoft
Kituo cha Upakuaji 
Tafutizi
Muundo Mahiri Tafutizi

Kipeto Lugha cha Kiolesura cha Windows 7

Ufafanuzi Mfupi
Kipeto Lugha cha Kiolesura cha Windows 7 (LIP) hutoa toleo lililofasiriwa nusu la Kiolesura cha Mtumiaji cha maeneo yanayotumika sana ya Windows 7

Kwenye Ukurasa Huu

Maelezo ya Haraka
Toleo:1.0
Tarehe Iliyochapishwa:14/01/2011
Lugha:Kiswahili
Saizi ya Upakuaji:2.5 MB - 6.5 MB*
*Saizi ya upakuaji inategemea vijenzi vilivyochaguliwa vya kupakuliwa.

Badili Lugha:
  

Muhtasari

Kipeto Lugha hiki Kiolesura cha Windows (LIP) hutoa toleo lililofasiriwa nusu la maeneo yanayotumika sana ya Windows. Baada ya kusanidi LIP, matini katika vigagula, vikasha ongezi, menyu, na mada za Msaada na auni zitaangazishwa katika lugha ya LIP. Matini ambayo hayajatafsiriwa yatakuwa katika lugha msingi ya Windows 7. Kwa mfano, kama ulinunua toleo la Kihispania la Windows 7, na ukasanidi LIP ya Kikatalani, matini mengine yatabaki katika Kihispania. Unaweza kusanidi zaidi ya LIP moja kwa lugha moja msingi. LIPs za Windows zinaweza kusanidiwa kwa matoleo yote ya Windows 7.

 Juu ya ukurasa

Mahitaji ya Mfumo

  • Mifumo ya Uendeshaji Inayokubaliwa: Windows 7
• Microsoft Windows 7
• Usanidi wa lugha msingi unaohitajika wa Windows 7: Kiingereza
• 4.63 Mb ya nafasi huru ya kupakua
• 15 Mb ya nafasi huru ya kusanidi

 Juu ya ukurasa

Maagizo

ONYO: Kama una usimbaji fiche wa BitLocker uliowezeshwa, tafadhali usitishe kabla ya kusanidi LIP. Fungua Control Panel, teua System and Security, kisha BitLocker Drive Encryption. Bofya kwenye Suspend Protection.

Kwa sababu kuna vipakuaji vya kando vya matoleo ya 32-biti na 64-biti vya Windows 7 LIP, kabla ya kuanza kupakua, unahitaji kubainisha ni toleo lipi la Windows 7 ulilosanidi. Hivi ndivyo unavyostahili kubainisha ni toleo lipi la Windows 7 ulilosanidi:

Bofya kwenye kitufe Start kisha bofya kulia kwenye Ngamizi na uteue Properties. Hii italeta maelezo msingi kuhusu ngamizi yako.
Angalia katika sehemu ya Mfumo ya aina ya Mfumo. Hii itaashiria kama Mfumo wako Endeshi wa Windows 7 ni Mfumo Endeshi wa 32-biti au kama ni Mfumo Endeshi wa 64-biti.

Kusanidi toleo la biti-32, aidha unaweza:

  1. Bofya kitufe cha Download, kisha bonyeza Open ili kusanidi LIP


  2. au

  3. Bofya Download pakua
    • Bofya Save ili kunakili jalada kwenye ngamizi yako,
    • Abiri kwa jalada lililopakuliwa na ulibofye mara mbili ili kusanidi LIP

Kusanidi toleo la biti-64, lazima utumie chaguo la 2 hapo juu.

 Juu ya ukurasa

Majalada kwenye Upakuaji Huu

Viungo katika sehemu hii hulingana na majalada ya kando yanayopatikana katika upakuaji huu. Pakua majalada yanayokufaa.
Jina la Jalada:Saizi ya Jalada

LIP_sw-KE-32bit.mlc

2.5 MB

LIP_sw-KE-64bit.mlc

4.0 MB

 Juu ya ukurasa

 Juu ya ukurasa


©2013 Microsoft Corporation. Haki zote zimehifadhiwa. Wasiliana Nasi |Kanuni za Matumizi |Alama za biashara |Taarifa ya Siri