Mifumo ya Uendeshaji Inayokubaliwa: Windows XP Service Pack 2
Programu inayohitajika: Toleo la Kiingereza (Marekani) la nui yoyote ya Office 2003 – kwa mfano Nui ya Kitaaluma ya Microsoft Office 2003 au Nui ya Kawaida ya Microsoft Office 2003 — au Toleo la Kiingereza (Marekani) la programu binafsi ya Office 2003 inayoauni Office 2003 ya Kipeto cha Kiolesura cha Kiswahili — Excel 2003, Outlook 2003, PowerPoint 2003, au Word 2003.
Office 2003 ya Kipeto cha Kiolesura cha Kiswahili inaweza pia kusanidiwa kwa Microsoft Office 2003 ya Kipeto cha Kiolesura cha Mtumiaji wa Lugha Nyingi kwa auni ya Kiingereza (Marekani).
Mahitaji ya Nafasi ya Diski: Mbali ya nafasi kwenye diski kuu inayotumiwa na programu za Office 2003 zilizosanidiwa kwa sasa, megabaiti (MB) 10 za nafasi ya diski kuu zinahitajika.
Pakua jalada la LIP.exe
kwa kubofya kitufe Pakua (juu) na kuakibisha jalada kwenye diski kuu yako.
Bofya maradufu jalada programu LIP.exe Kwenye diski kuu yako kuanzisha programu Muundo.
Fuata maelekezo kwenye kiwamba kukamilisha usanidi.
Maelekezo kwa utumizi:
Kufungua Kiolesura cha Mtumiaji kwenye lugha ya Kipeto cha Kiolesura cha Kiswahili cha Office 2003, fuata hatua hizi zifuatazo:
Kwenye menyu ya Anza Elekeza kielekezi kwenye Programu Zote, kisha elekeza kwenye Microsoft Office, elekeza kwenye Zana za Microsoft Office, na kisha bofya Mipangizo ya Lugha ya Microsoft Office 2003.
Kwenye kichupo cha Kiolesura cha Mtumiaji na Saidia
katika Angazisha Office 2003 katika orodha, teua lugha unayotaka kuangazisha.
Bofya Sawa.
Mipangizo ya lugha unayoteua itafanya kazi mara nyingine utakapoanzisha programu za Office.
Kuondoa Pakua hii:
Toka kwenye programu zote.
Kwenye menyu ya Anza elekeza kielekezi kwenye Mipangizo kisha Paneli Dhibiti.
Bofya maradufu Ongeza/Ondoka Programu.
Katika orodha ya programu zilizosanidiwa hadi sas, bofya Kipeto cha Kiolesura cha Kiswahili ya Microsoft Office 2003, kisha bofya Ondoa or Ongeza/Ondoa. Kama kisanduku ongezi kinatokea, fuata maelekezo ya kuondoa programu.
Bofya Ndiyo au Sawa Kuthibitisha kuwa unataka kuondoa programu