Office

  Microsoft Office Language Interface Pack 2010 – Kiswahili

  Badili Lugha:
  Microsoft Office Language Interface Pack 2010 – Kiswahili hutoa kiolesura cha mtumiaji cha Kiswahili kwa programu nyingi za Microsoft Office 2010.
  • Note:There are multiple files available for this download.Once you click on the "Download" button, you will be prompted to select the files you need.
   Toleo:

   1

   Jina la Jalada:

   languageinterfacepack-x86-sw-ke.exe

   languageinterfacepack-x64-sw-ke.exe

   O14LipHelp-sw-ke.chm

   Tarehe Iliyochapishwa:

   5/23/2011

   Saizi ya Jalada:

   13.3 MB

   14.7 MB

   207 KB

    Microsoft Office Language Interface Pack 2010 – Kiswahili hutoa kiolesura cha mtumiaji cha Kiswahili kwa:
    • Microsoft Office Excel 2010

    • Microsoft Office OneNote 2010

    • Microsoft Office Outlook 2010

    • Microsoft Office PowerPoint 2010

    • Microsoft Office Word 2010
  • Mifumo ya Uendeshaji Inayokubaliwa:

   Windows 7, Windows Vista, Windows XP

    • Programu i/zinahitajika: Toleo lolote au nakala ya kipekee ya Microsoft Office 2010 iliyo na programu-tumizi mojawapo au zaidi zifuatazo: Excel, OneNote, Outlook, PowerPoint au Word.
    • Mahitaji ya nafasi diski: Zaidi ya nafasi ya diski kuu iliyotumika katika kusakinishwa kwa programu za Office 2010 kwa sasa, ni lazima megabaiti (MB) 20 za nafasi ya diski kuu zipatikane.
   • Ili kusakinisha kipakuzi hiki:
    1. Pakua faili la LanguageInterfacePack.exe kwa kubofya kitufe cha Pakua (hapo juu) na kuhifadhi faili katika diski kuu yako
    2. Bofya mara mbili faili la programu LanguageInterfacePack.exe katika diski kuu yako ili kuanza programu ya Usanidi.
    3. Fuata maagizo katika skrini ili kumaliza usakinishaji.
    4. Baada ya kusakinishwa, faili Nisome lako la Microsoft Office 2010 Language Interface Pack linaweza kupatikana katika C:\Program Files\Common Files\microsoft shared\OFFICE14\LCID\LIPread.htm
    5. Upandishaji daraja wa Office 2007 na Office 2010 Language Interface Pack 2007, au toleo kabla ya Office 2010 na Office Language Interface Pack 2010, hautegemezwi. Kama unataka kupandisha daraja la usakinishaji wa msingi wa Office 2007 hadi uwe na Office 2010 pamoja na Office Language Interface Pack 2010, unahitajika:
     • Sakinusha Office 2007 Language Interface Pack
     • Endesha usanidi wa Office 2010 na chagua chaguo la kupandisha daraja.
     • Wakati usanidi wa Office 2010 umekamilika, sakinisha na sanidi Office 2010 Language Interface Pack


     • Kuamilisha bidhaa yako ya Office:
     • Kama unalo tatizo katika kusoma Msimbo wa Usakinishaji wote katika kidadisi cha "Microsoft Office Activation Wizard" , au msimbo wote wa usakinishaji hauonyeshi kwa usahihi wakati unatumia Microsoft® Office Language Interface Pack 2010, tafadhali katisha sogora na badilisha kutumia Kiingereza cha bidhaa ili kuamilisha bidhaa yako ya Microsoft Office.


    Maagizo ya kutumia:

    Ili kubadilisha Kiolesura cha Mtumiaji chako hadi katika Microsoft Office Language Interface Pack 2010 – Kiswahili, fuata hatua hizi:

    1. Zindua Mapendeleo ya Lugha ya Microsoft Office 2010 kutoka menyu Anza\Programu Zote\Microsoft Office\Zana za Microsoft Office
    2. Chini ya Chagua Lugha za Uonyesho na Msaada,chini ya Lugha ya Uonyesho teua lugha inayohitajika na bofya katika kitufe cha Weka kama Chaguo-msingi
    3. Chini ya Chagua Lugha za Uhariri,chagua lugha inayohitajika na bofya katika kitufe cha Weka kama Chaguo-msingi
    4. Bofya kitufe Sawa

    Mipangilio ya lugha uliyoteua itawekwa kwa matumizi wakati mwingine utakapoanza programu zako za Office.
    Dokezo: Msaada hauwezi kubadilishwa katika Microsoft Office Language Interface Pack 2010 – Kiswahili. Msaada utabaki kila wakati katika lugha asilia ya usakinishaji wako.
    Kila wakati weka msaada wa uonyesho wako katika orodha kunjuzi hadi katika lugha msingi.

    Ili kuondoa kipakuzi hiki:
     Fuata hatua hizi katika matoleo ya Windows XP Home au Professional:
    1. Aga programu zote.
    2. Bofya mara mbili ikoni ya Ongeza au Ondoa Programu katika Paneli Dhibiti ya Windows
    3. Bofya Microsoft Office Language Interface Pack 2010 katika kisanduku cha Programu zilizosakinishwa kwa sasa, na kisha bofya kitufe Ondoa
    4. Fuata maagizo katika skrini.

     Fuata hatua hizi katika Windows Vista au Windows 7:
    1. Aga programu zote.
    2. Bofya mara mbili ikoni ya Programu na Vipengele katika Paneli Dhibitiya Windows.
    3. Kwenye chaguo la Sakinusha au Badilisha Programu, bofya Microsoft Office Language Interface Pack 2010 –Kiswahili kwenye kisanduku cha Programu zilizosakinishwa kwa sasa, na kisha teua chaguo la Sakinusha .
    4. Fuata maagizo katika skrini.    Ikiwa huwezi kuona maudhui ya faili ya CHM baada ya kuipakua, unaweza kuendesha hatua zifuatazo zitakazokuwezesha kutazama maudhui:
    1. Fungua folda ambapo ulipakua faili ya CHM
    2. Bofya kulia kwenye CHM na kutoka kwenye menyu ambayo inatokea,teua.
    3. Kwenye General tab, bofya kitufe cha Unblock button kisha ubofye kitufe cha Sawa.
    4. Bofya mara mbili kwenye faili ya CHM na sasa utaweza kuona maudhui yake.

  Vipakuaji Maarufu

  Loading your results, please wait...

  Visasisho vya kompyuta bila malipo

  • Mipachiko ya usalama
  • Visasisho vya programu
  • Furushi za huduma
  • Viendeshi vya maunzi