Ilichapishwa:
Yataanza kutumika: Tarehe 1 Mei, 2018
Makubaliano ya Huduma ya Microsoft
Faragha YakoFaragha Yako1_YourPrivacy
Muhtasari

1. Faragha Yako. Faragha yako ni muhimu kwetu. Tafadhali soma Taarifa ya Faragha ya Microsoft ("Taarifa ya Faragha") kwa kuwa inafafanua aina ya data tunayokusanya kutoka kwako na vifaa vyako ("Data"), jinsi tunavyotumia Data yako, na misingi ya kisheria tunayo ya kuchakata Data yako. Taarifa ya Faragha hufafanua pia jinsi Microsoft hutumia maudhui yako, ambayo ni mawasiliano yako na wengine; machapisho au maoni yaliyowasilishwa na wewe kwa Microsoft kupitia Huduma; na faili, picha, nyaraka, na sauti, kazi za kidijitali, mitiririko ya moja kwa moja na video ambazo unazopakia, kuhifadhi, kutangaza au kushiriki kupitia Huduma ("Maudhui Yako"). Wakati uchakataji unategemea kibali na kwa kadri inayoruhusiwa na sheria, kwa kutumia Huduma au kukubaliana na Masharti haya, unatoa kibali kwa Microsoft kukusanya, kutumia na kufichua Maudhui na Data yako kama ilivyofafanuliwa katika Taarifa ya Faragha. Katika hali nyingine, tutakupa ilani tofauti na kuomba kibali chako kama iliyorejelewa katika Taarifa ya Faragha.

Maandishi kamili
Maudhui YakoMaudhui Yako2_yourContent
Muhtasari

2. Maudhui Yako. Nyingi ya Huduma zetu hukuwezesha kuhifadhi au kushiriki Maudhui yako au kupokea nyenzo kutoka kwa wengine. Hatudai umiliki wa Maudhui Yako. Maudhui yako yanabakia kuwa Maudhui Yako, na unawajibika.

 • a. Wakati unaposhiriki Maudhui Yako na watu wengine, unafahamu kwamba wanaweza, mahali popote duniani, kutumia, kuhifadhi, kurekodi, kuzalisha upya, kutangaza, kupitisha, kushiriki na kuonyesha (na kwenye HealthVault, kufuta) Maudhui yako bila kukufidia. Ikiwa hutaki wengine kuwa na uwezo huo, usitumie Huduma kushiriki Maudhui Yako. Unakubali na kuhakikisha kwamba kwa muda wa Masharti haya, una (na utakuwa) na haki zote zinazostahili kwa Maudhui Yako unayopakia, kuhifadhi, au kushiriki kwenye au kupitia Huduma na kwamba mkusanyiko, matumizi, na ubakizaji wa Maudhui Yako hayatakiuka sheria au haki zozote za wengine. Microsoft haimiliki, kudhibiti, kuthibitisha, kulipia, kuidhinisha au kuchukua uwajibikaji wowote wa Maudhui Yako na haiwezi kuwajibika kwa Maudhui Yako au nyenzo zilizopakiwa, kuhifadhiwa au kushirikiwa na wengine kwa kutumia Huduma.
 • b. Kwa umbali unaofaa ili kutoa Huduma kwako na kwa wengine, ili kukulinda wewe na Huduma, na kuboresha bidhaa na huduma za Microsoft, unaipa Microsoft leseni ya rasilimali ya akili isiyokuwa na mrahaba na ya duniani kote ya kutumia Maudhui Yako, kwa mfano, kutoa nakala, kubakiza, kupitisha, kuumbiza upya, kuonyesha, na kusambaza kupitia zana za mawasiliano Maudhui Yako kwenye Huduma. Ukichapisha Maudhui Yako katika maeneo ya Huduma ambayo yanapatikana sana mtandaoni bila vizuizi, huenda Maudhui Yako yakatokea katika maonyesho au nyenzo ambazo zinakuza Huduma. Baadhi ya Huduma zinakubaliwa kwa utangazaji. Vidhibi vya jinsi Microsoft inavyobinafsisha utangazaji vinapatikana kwenye ukurasa wa Usalama na faragha wa tovuti ya usimamizi wa akaunti ya Microsoft. Hatutumii unachokisema katika barua pepe, soga, simu za video au barua ya sauti, au nyaraka, picha au faili nyingine zako za kibinafsi kulenga matangako kwako. Sera zetu za utangazaji zimeshughulikiwa kwa undani katika Taarifa ya Faragha.
Maandishi kamili
Kanuni ya Maadili MemaKanuni ya Maadili Mema3_codeOfConduct
Muhtasari

3. Kanuni ya Maadili Mema.

 • a. Kwa kukubaliana na Masharti haya, unakubali kwamba, wakati unatumia Huduma, utafuata kanuni hizi:
  • i. Usifanye kitu chochote ambacho ni kinyume cha sheria
  • ii. Usihusike katika shughuli yoyote ambayo inawatumia vibaya, kuwadhuru, au kuwatisha watoto.
  • iii. Usitume barua taka. Barua taka ni barua pepe, machapisho, maombi ya mawasiliano, SMS (ujumbe wa maandishi), au ujumbe wa papo hapo ambao hautakikani au usioombwa.
  • iv. Usionyeshe hadharani au kutumia Huduma kushiriki maudhui au nyenzo zisizofaa (ikiwa ni pamoja na, kwa mfano, uchi, unyama, ponografia, lugha yenye kuudhi, picha za kukera, au shughuli ya uhalifu) au Maudhui Yako au nyenzo ambazo hazifuati sheria au masharti ya eneo lako.
  • v. Usihusike katika shughuli ambayo ni ya ulaghai, uongo au ya kupotosha (k.m. kuomba pesa kwa kujifanya, kumuiga mtu mwingine, kuhadaa Huduma ili kuongeza hesabu ya kucheza, au kuathiri cheo, ukadiriaji, au maoni) au kashifu au kuharibu jina.
  • vi. Usibadilishe vizuizi vyovyote vya ufikiaji au upatikajani wa Huduma.
  • vii. Usihusike katika shughuli ambayo inakuathiri wewe, Huduma au wengine (k.m. kusambaza virusi, unyemeleaji, kuchapisha maudhui ya ugaidi, kusema maneno ya chuki, au yanayohimiza uhasama dhidi ya wengine).
  • viii. Usikiuke haki za wengine (k.m. kushiriki muziki wenye hakimiliki au nyenzo zingine zenye hakimiliki bila idhini, kuuza tena au kusambaza ramani za Bing, au picha).
  • ix. Usihusike katika shughuli ambayo inakiuka faragha au haki za kulinda data za wengine.
  • x. Usiwasaidie wengine kuvunja sheria hizi.
 • b. Utekelezaji. Ukikiuka Masharti haya, tunaweza, kwa uamuzi wetu, kukomesha kutoa Huduma kwako au tunaweza kufunga akaunti yako ya Microsoft. Huenda pia tukazuia uwasilishaji wa mawasiliano (kama vile barua pepe, kushiriki faili au ujumbe wa papo hapo) kwenda au kutoka kwa Huduma katika juhudi za kutekeleza Masharti haya, au tunaweza kuondoa au kukataa kuchapisha Maudhui Yako kwa sababu yoyote ile. Wakati unachunguza ukiukaji unaowezekana wa Masharti haya, Microsoft inahifadhi haki ya kuhakiki Maudhui Yako ili kutatua tatizo, na unatoa idhini ya hakiki kama hiyo. Hata hivyo, hatuwezi kufuatilia Huduma zote na hatutajaribu kufanya hivyo.
 • c. Matumizi ya Huduma za Xbox. Bofya hapa kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi Kanuni hii ya Maadili mema inavyotumika kwenye Xbox Live, Michezo ya Windows Live na michezo ya Microsoft Studios, programu, huduma na maudhui yanayotolewa na Microsoft. Ukiukaji wa Kanuni ya Maadili Mema kupitia Huduma za Xbox (uliofafanuliwa katika sehemu ya 13(a)(i)) kunaweza kusababisha kusitishwa au kupigwa marufuku kushiriki katika Huduma za Xbox, ikiwa ni pamoja na kuondolewa kwa leseni za maudhui, muda wa Uanachama wa Xbox Gold, na masalio ya akaunti ya Microsoft yanayohusishwa na akaunti.
Maandishi kamili
Kutumia Huduma na UsaidiziKutumia Huduma na Usaidizi4_usingTheServicesSupport
Muhtasari

4. Kutumia Huduma na Usaidizi.

 • a. Akaunti ya Microsoft. Utahitaji Akaunti ya Microsoft ili kufikia nyingi ya Huduma hizi. Akaunti yako ya Microsoft hukuwezesha kuingia kwenye bidhaa, tovuti na huduma zinazotolewa na Microsoft na baadhi ya washirika wa Microsoft.
  • i. Kufungua Akaunti. Unaweza kufungua akaunti ya Microsoft kwa kujiandikisha mtandaoni. Unakubali kutotumia maelezo yoyote ya uongo, yasiyo sahihi au ya kupotosha wakati unajiandikisha kwa akaunti yako ya Microsoft. Katika hali nyingine, mhusika mwingine kama vile mtoa huduma wako wa Intaneti, huenda amakuwekea akaunti ya Microsoft. Ikiwa ulipokea akaunti yako ya Microsoft kutoka kwa mhusika mwingine, huenda mhusika huyo mwingine akawa na haki za ziada kwa akaunti yako, kama vile uwezo wa kufikia au kufuta akaunti yako ya Microsoft. Tafadhali hakiki masharti yoyote ya ziada ambayo mhusika mwingine amekupa, kwa kuwa Microsoft haiwajibiki kuhusiana na masharti haya ya ziada. Ukifungua akaunti ya Microsoft kwa niaba ya shirika, kama vile biashara au mwajiri wako, unahakikisha kwamba una mamlaka ya kisheria ya kufunga shirika hilo kwa Masharti haya. Huwezi kuhamisha hati tambulisho zako za akaunti ya Microsoft kwa mtumiaji au shirika lingine. Ili ulinde akaunti yako, weka maelezo na nywila ya akaunti yako siri. Unawajibika kwa shughuli zote zinazofanyika chini ya akaunti yako ya Microsoft.
  • ii. Matumizi ya Akaunti. Lazima utumie akaunti yako ya Microsoft ili iendelee kutumika. Hii humaanisha lazima uingie angalau mara moja kwa kipindi cha miaka mitano ili akaunti yako ya Microsoft, na Huduma husika ziendelee kutumika, isipokuwa iwe imesemwa kivingine katika ofa ya sehemu iliyolipwa ya Huduma. Ukikosa kuingia wakati huu, tutachukulia kwamba akaunti yako ya Microsoft haitumiki na tufaifunga kwa niaba yako. Tafadhali angalia sehemu ya 4(a)(iv)(2) kwa matokeo ya akaunti iliyofungwa ya Microsoft. Lazima uingie kwenye kisanduku pokezi chako cha Outlook na OneDrive yako (kando) angalau mara moja kwa kipindi cha mwaka mmoja, kama sivyo tufafunga kisanduku pokezi chako cha Outlook.com na OneDrive yako kwa niaba yako. Lazima uingie katika Huduma za Xbox angalau mara moja katika kipindi cha miaka mitano ili kudumisha lebo ya mchezaji inayohusishwa na akaunti yako ya Microsoft. Tukishuku kwamba akaunti yako ya Microsoft inatumiwa na mhusika mwingine kwa ulaghai (kwa mfano, kama matokeo ya akaunti kuhatarishwa), huenda Microsoft ikasitisha akaunti yako hadi uweze kudai umiliki. Kutegemea hali ya uvamizi, huenda tukahitajika kuzima idhini ya kufikia baadhi au Maudhui Yako yote. Ikiwa una tatizo la kufikia akaunti yako ya Microsoft, tafadhali tembelea tovuti hii: https://go.microsoft.com/fwlink/?LinkId=238656.
  • iii. Watoto na Akaunti. Kwa kutumia Huduma, unamaanisha kwamba umefikia umri wa "wengi" au "majukumu ya kisheria" ya unakoishi au una mzazi halali au mlezi wa kisheria ambaye ametoa kibali kufungwa na Masharti haya. Ikiwa hujui kama umefikia umri wa wengi au "majukumu ya kisheria" ya unakoishi, au hufahamu sehemu hii, tafadhali omba mzazi au mlezi wako wa kisheria kwa msaada na kibali kabla ya kufungua akaunti ya Microsoft. Ikiwa wewe ni mzazi au mlezi wa kisheria wa mtoto ambaye amefungua akaunti ya Microsoft, wewe na mtoto mnakubali kufungwa na Masharti haya na mnawajibika kwa matumizi yote ya akaunti ya Microsoft au Huduma, ikiwa ni pamoja na ununuzi, iwe akaunti ya mtoto imefunguliwa kwa sasa au imefunguliwa baadaye.
  • iv. Kufunga Akaunti Yako.
   • 1. Unaweza kukatisha Huduma fulani au kufunga akaunti yako ya Microsoft wakati wowote kwa sababu yoyote ile. Ili ufunge akaunti yako ya Microsoft, tafadhali tembelea https://go.microsoft.com/fwlink/p/?linkid=618278. Wakati unatuomba tufunge akaunti yako ya Microsoft, tutaiweka katika hali ya kusitishwa kwa siku 60 iwapo utabadilisha nia. Baada ya kipindi cha siku 60, akaunti yako ya Microst itafungwa. Tafadhali angalia sehemu ya 4(a)(iv)(2) hapa chini kwa ufafanuzi wa kinachofanyika wakati akaunti yako ya Microsoft inafungwa. Kuingia tena wakati wa kipindi cha siku 60, kutaamilisha tena akaunti yako ya Microsoft.
   • 2. Ikiwa akaunti yako ya Microsoft imefungwa (iwe ni wewe au sisi), mambo machache hufanyika. Kwanza, haki yako ya kutumia akaunti ya Microsoft kufikia Huduma hukoma mara moja. Pili, tutafuta Data au Maudhui Yako yanayohusishwa na akaunti yako ya Microsoft au tutaitenganisha na wewe na akaunti yako ya Microsoft (isipokuwa iwe tunahitajika na sheria kuiweka, kuirejesha, au kuihamisha kwako au mhusika mwingine uliyemtambua). Unastahili kuwa na mpango wa chelezo wa mara kwa mara kwa kuwa Microsoft haitaweza kuepua Maudhui au Data yako akaunti yako ikifungwa. Tatu, unaweza kupoteza ufikiaji wa bidhaa ulizopata.
 • b. Akaunti za Kazini au Shuleni. Unaweza kuingia katika huduma nyingine za Microsoft kwa kutumia anwani ya barua pepe ya kazini au shuleni. Ukifanya hivyo, unakubali kwamba mmiliki wa kikoa hicho kinachohusishwa na anwani yako ya barua pepe anaweza kudhibiti na kusimamia akaunti yako, na kufikia na kuchakata Data yako, ikiwa ni pamoja na maudhui ya mawasiliano na faili zako, na kwamba huenda Microsoft ikamwarifu mmiliki wa kikoa ikiwa akaunti au Data imehatarishwa. Unakubali zaidi kwamba matumizi yako ya huduma za Microsoft yanaweza kutegemea makubaliano ambayo Microsoft inayo na wewe au shirika lako na masharti haya hayatumiki. Ikiwa tayari una akaunti ya Microsoft na unatumia anwani tofauti ya barua pepe ya kazini au shuleni kufikia Huduma zinazoshughulikiwa chini ya Masharti haya, huenda ukaulizwa usasishe anwani ya barua pepe inayohusishwa na akaunti yako ya Microsoft ili uweze kuendelea kutumia Huduma kama hizo.
 • c. Vifaa vya Ziada/Mipango ya Data. Ili utumie Huduma nyingi, utahitaji muunganisho wa intaneti na/au data/mpango wa simu. Huenda pia ukahitaji vifaa vya ziada, kama vile vifaa vya kichwani, kamera au mairofoni. Unawajibika kutoa miunganisho yote, mipango, na vifaa vinavyohitajika ili utumie Huduma na kulipia ada zinazolipishwa na watoa huduma kwa miunganisho, mipango na vifaa vyako. Ada hizo zinaongezea ada zozote unazotulipa kwa Huduma na hatutakufikia kwa ada kama hizo. Wasiliana na mtoa huduma wako ili ubainishe kama kuna ada zozote kama hizo ambazo zinaweza kutumika kwako.
 • d. Arifa za Huduma. Wakati kuna kitu tunataka kukuelezea kuhusu Huduma unayotumia, tutakutumia arifa za Huduma. Ukitupatia anwani yako ya barua pepe au nambari ya simu inayohusiana na akaunti yako ya Microsoft, basi tunaweza kukutumia arifa za Huduma kupitia barua pepe au kupitia SMS (ujumbe wa maandishi), ikiwa ni pamoja na kudhibitisha kitambulisho chako kabla ya kusajili nambari yako ya simu ya mkononi. Tunaweza pia kukutumia arifu za Huduma kwa njia nyingine (kwa mfano kwa ujumbe katika ujumbe.) Ada ya data au ya kutuma ujumbe inaweza kutuma wakati unapokea arifa kupitia SMS.
 • e. Usaidizi. Usaidizi kwa wateja wa baadhi ya Huduma unapatikana kwenye support.microsoft.com. Huenda baadhi ya Huduma zikatoa usaidizi tofauti au wa ziada kwa wateja, kulingana na masharti yanayopatikana kwenye www.microsoft.com/support-service-agreement, isipokuwa iwe imeelezewa kivingine. Huenda usaidizi usipatikane kwa matoleo ya uhakiki au beta ya vipengele au Huduma. Huenda Huduma zisitangamane na programu au huduma iliyotolewa na wahusika wengine, na unawajibika kujifahamu na vifaa tangamanifu.
 • f. Kukatisha Huduma zako. Ikiwa Huduma zako zitakatishwa (na wewe au sisi), kwanza haki yako ya kufikia Huduma hukoma mara moja na leseni yako ya kutumia programu inayohusiana na Huduma zetu huisha. Pili, tutafuta Data au Maudhui Yako yanayohusishwa na Huduma yako ya Microsoft au tutaitenganisha na wewe na akaunti yako ya Microsoft (isipokuwa iwe tunahitajika na sheria kuiweka, kuirejesha, au kuihamisha kwako au mhusika mwingine uliyemtambua). Kama matokeo yake huenda usiweze tena kufikia Huduma yoyote (au Maudhui Yako ambayo umehifadhi kwenye Huduma hizo). Unapaswa kuwa na mpango wa kawaida wa chelezo. Tatu, unaweza kupoteza ufikiaji wa bidhaa ulizopata. Ikiwa umekatisha akaunti yako ya Microsoft na huna akaunti nyingine inayoweza kufikia Huduma, huenda Huduma zako zikakatishwa mara moja.
Maandishi kamili
Kutumia Programu na Huduma za Wahusika WengineKutumia Programu na Huduma za Wahusika Wengine5_usingThird-PartyAppsAndServices
Muhtasari

5. Kutumia Programu na Huduma za Wahusika Wengine. Huenda Huduma zikakuruhusu kufikia au kupata bidhaa, huduma, tovuti, viungo, maudhui, nyenzo, michezo, ujuzi, ujumuishaji, boti au programu kutoka kwa wahusika wengine huru (makampuni au watu ambao sio Microsoft) ("Programu na Huduma za Wahusika wengine"). Huduma zetu nyingi hukusaidia pia kutafuta, kuomba, au kuingiliana na Programu na Huduma za Wahusika wengine au kukuruhusu kushiriki Maudhui au Data yako, na unafahamu kwamba unaelekeza huduma zetu kukupa Programu na Huduma za Wahusika wengine. Programu na Huduma za Wahusika wengine zinaweza pia kuhifadhi Maudhui au Data Yako na mchapishaji, mtoa huduma au opereta wa Programu na Huduma za Wahusika wengine. Huenda Programu na Huduma za Wahusika Wengine zikakupa sera ya faragha au zikahitaji ukubali masharti ya ziada kabla uweze kusakinisha au kutumia Programu au Huduma za Wahusika Wengine. Angalia sehemu ya 13(b) kwa masharti ya ziada ya programu yanayohitajika kupitia Duka la Office, Duka la Xbox au Duka la Windows. Unastahili kuhakiki masharti yoyote ya ziada na sera za faragha kabla ya kupata, kutumia, kuomba, au kuunganisha Akaunti yako ya Microsoft kwenye Programu na Huduma zozote za Wahusika wengine. Masharti yoyote ya ziada hayarekebishi Masharti haya. Microsoft haikupi leseni ya rasilimali yoyote ya akili kama sehemu ya Programu na Huduma yoyote ya Wahusika wengine. Unakubali kuwajibika kwa hatari na dhima zote zinazotokana na matumizi yako ya Programu na Huduma hizi za Wahusika Wengine na kwamba Microsoft haitawajibika kwa matatizo yoyote yanayotokana na matumizi yake. Microsoft haitawajibika kwako au wengine kwa maelezo au huduma zinazotolewa na Programu na Huduma zozote za Wahusika Wengine.

Maandishi kamili
Upatikanaji wa HudumaUpatikanaji wa Huduma6_serviceAvailability
Muhtasari

6. Upatikanaji wa Huduma.

 • a. Huduma, Programu na Huduma za Wahusika Wengine, au nyenzo au bidhaa zinazotolewa kupitia huduma zinaweza kutopatikana mara kwa mara, zinaweza kutolewa kwa muda, au zinaweza kutofautiana kulingana na eneo au kifaa chako. Ukibadilisha eneo linalohusishwa na akaunti yako ya Microsoft, huenda ukahitaji kupata upya nyenzo au programu ambazo zilipatikana kwako na kulipiwa katika eneo lako la awali. Unakubali kutofikia au kutumia nyenzo au Huduma ambazo ni kinyume cha sheria au ambazo hazina leseni ya kutumiwa nchini ambazo unafikia au kutumia Nyenzo au Huduma kama hizo, au kuficha au kuwakilisha vibaya eneo au kitambulisho chako ili kufikia au kutumia nyenzo au Huduma kama hizo.
 • b. Tunajizatiti kuhakikisha Huduma zinafanya kazi; hata hivyo, huduma zote za mtandaoni wakati mwingine hukabiliana na matatizo na upungufu, na Microsoft haiwajibiki kwa usumbufu wowote au hasara unayoweza kupata kama matokeo yake. Katika tukio la kutofanya kazi, huenda usiweze kuepua Maudhui au Data Yako ambayo umehifadhi. Tunapendekeza kwamba ucheleze mara kwa mara Maudhui na Data yako ambayo unahifadhi kwenye huduma au kuhifadhi kwa kutumia Programu na Huduma za Wahusika Wengine.
Maandishi kamili
Visasisho vya Huduma au Programu, na Mabadiliko kwa Masharti HayaVisasisho vya Huduma au Programu, na Mabadiliko kwa Masharti Haya7_updatesToTheServicesOrSoftwareAndChangesToTheseTerms
Muhtasari

7. Visasisho vya Huduma au Programu, na Mabadiliko kwa Masharti Haya.

 • a. Tunaweza kubadilisha Masharti haya wakati wowote, na tutakueleza tukifanya hivyo. Kwa kutumia Huduma baada ya mabadiliko kuanza kutumika humaanisha unakubaliana na masharti mapya. Ikiwa hukubaliani na masharti mapya, lazima ukome kutumia Huduma, ufunge akaunti yako ya Microsoft na, ikiwa wewe ni mzazi au mlezi, umsaidie mtoto wako kufunga akaunti yake ya Microsoft.
 • b. Wakati mwingine unahitaji visasisho vya programu ili uendelee kutumia Huduma. Tunaweza kukagua toleo lako la programu kiotomatiki na kupakua visasisho vya programu au mabadiliko ya usanidi. Unaweza pia kuhitajika kusasisha programu ili uendelee kutumia Huduma. Visasisho kama hivyo hulingana na Masharti haya isipokuwa masharti mengine yawe yameandamana, ambapo masharti hayo mengine yatatumika. Microsoft haiwajibiki kutekeleza visasisho vyovyote vipatikane na haihakikishi kwamba tutaunga mkono toleo la mfumo ulilonunua au ambalo umepokea leseni ya programu, maudhui au bidhaa nyingine. Visasisho kama hivyo huenda visitangamane na programu au huduma zinazotolewa na wahusika wengine. Unaweza kuondoa kibali chako cha visasisho vya baadaye ya vya programu wakati wowote kwa kusanidua programu.
 • c. Kwa kuongezea, huenda kukawa na nyakati ambapo tutahitaji kuondoa au kubadilisha vipengee au utendakazi wa Huduma au kukomesha kutoa Huduma au kufikia Programu na Huduma za Wahusika wengine kwa pamoja. Isipokuwa kwa kiasi unachohitajika na sheria husika, hatuna majukumu yoyote ya kutoa upakiaji upya au mbadala wa nyenzo, Bidhaa zozote za Dijitali (zilizofafanuliwa katika sehemu ya 13(k)), au programu zilizonunuliwa awali. Huenda tukatoa Huduma au vipengele vyake katika mwonekano awali au toleo la beta, ambayo huenda isifanye kazi vizuri au kwa njia sawa kama vile toleo la mwisho lingeweza kufanya kazi.
 • d. Ili uweze kutumia nyenzo zinazolindwa na Usimamiaji wa haki za dijitali za (DRM), huenda baadhi ya muziki, michezo, filamu, vitabu na zaidi, huenda programu ya DRM ikawasiliana kiotomatiki na seva ya haki mtandaoni na kupakua na kusakinisha visasisho vya DRM.
Maandishi kamili
Leseni ya ProgramuLeseni ya Programu8_softwareLicense
Muhtasari

8. Leseni ya Programu. Isipokuwa iwe pamoja na makubaliano tofauti ya leseni ya Microsoft (kwa mfano, ikiwa unatumia programu ya Microsoft ambayo imejumuishwa na ni sehemu ya Windows, basi Masharti ya Leseni ya Programu za Microsoft ya Mfumo wa Uendeshaji wa Windows husimamia programu), programu yoyote inayotolewa na sisi kwako kama sehemu ya Huduma hutegemea Masharti haya. Programu zilizopatikana kupitia Office Store, Windows Store na Xbox Store zitategemea sehemu ya 13(b)(i) hapa chini.

 • a. Ukiafikiana na Masharti haya, tunakupa haki ya kusakinisha na kutumia nakala moja ya programu kwa kila kifaa mahali popote duniani kwa matumizi ya mtu mmoja tu kwa wakati mmoja kama sehemu ya matumizi yako ya Huduma. Kwa vifaa vingine, programu kama hiyo inaweza kusakinishwa mapema, kwa matumizi yako ya kibinafsi, yasiyo ya kibiashara ya Huduma. Programu au tovuti ambayo ni sehemu ya Huduma inaweza kujumuisha msimbo wa mhusika mwingine. Hati au msimbo wowote wa mhusika mwingine, uliohusishwa au kurejelewa kutoka kwenye programu au tovuti, unapewa leseni na wahusika wengine ambao wanamiliki msimbo huo, sio Microsoft. Ilani, zikiwa zipo, za mhusika wa mwingine zimejumuishwa kwa maelezo yako tu.
 • b. Programu imepewa leseni, haiuzwi, na Microsoft inahifadhi haki zote za programu ambazo hazijatolewa moja kwa moja na Microsoft, iwe kwa kudokeza, ushahidi au kivingine vile. Leseni hii haikupi haki yoyote, na huenda usiweze:
  • i. kubadilisha au kuruka hatua zozote za ulinzi wa kiteknolojia au zinazohusiana na programu au Huduma;
  • ii. kubomoa, kufichua, kusimbua, kufikia bila idhini, kuiga, kutumia vibaya, au kugeuza uhandisi wa programu yoyote au hali nyingine ya Huduma ambayo imejumuishwa au inayoweza kufikiwa kupitia Huduma, isipokuwa na kwa umbali tu uliokubaliwa na sheria ya hakimiliki kama inaruhusu kufanya hivyo;
  • iii. kugawanya vijenzi vya programu au Huduma ili kutumiwa na vifaa tofauti;
  • iv. kuchapisha, kunakili, kukodisha, kukomboa, kuuza, kuuzanje, kuletanchini, kusambaza, au kuazima programu au Huduma, isipokuwa Microsoft ikuidhiinishe kufanya hivyo;
  • v. kuhamisha programu, leseni zozote za programu, au haki zozote za kufikia au kutumia Huduma;
  • vi. kutumia Huduma kwa njia yoyote isiyoidhinishwa ambayo inaweza kuingiliana na matumizi ya mtu mwingine au kufikia huduma yoyote, data, akaunti, au mtandao.
  • vii. usiweze kufikia Huduma au kurekebisha kifaa chochote kilichoidhinishwa cha Microsoft (k.m., Xbox One, Xbox 360, Microsoft Surface, n.k..) na programu zisizoidhinishwa za wahusika wengine.
Maandishi kamili
Masharti ya MalipoMasharti ya Malipo9_paymentTerms
Muhtasari

9. Masharti ya Malipo. Ikiwa ulinunua Huduma, basi masharti haya ya malipo yanatumika kwa ununuzi wako na unakubaliana nayo.

 • a. Gharama. Ikiwa kuna gharama inayohusishwa na sehemu ya Huduma, unakubali kulipa gharama hiyo katika sarafu iliyobainishwa. Bei iliyoandikwa ya Huduma haijumuishi kodi zote zinazohusika na ada ya ubadilishaji sarafu, isipokuwa iwe imeelezewa. Bei zote za bidhaa zilizolipwa za Skype zinajumuisha ushuru husika, isipokuwa iwe imesemekana kivingine. Unawajibika kivyako kulipia kodi kama hizo au gharama nyingine. Skype uhesabu ushuru kulingana na anwani ya makazi inayohusishwa na maelezo yako kutoza bili. Unawajibika kuhakikisha kwamba anwani hii imesasishwa na ni sahihi. Isipokuwa kwa bidhaa za Skype, ushuru uhesabiwa kulingana na eneo lako wakati akaunti yako ya Microsoft ilisajiliwa isipokuwa sheria za nchini zinahitaji msingi tofauti wa hesabu. Huenda tukasitisha au kukatisha Huduma tukikosa kupokea malipo kamili kwa wakati unaofaa kutoka kwako. Usitishaji au kukatishwa kwa Huduma kwa ajili ya kutokulipa kunaweza kusababisha kupoteza ufikiaji na matumizi ya akaunti yako na maudhui yake. Kuunganisha kwenye Intaneti kupitia mtandao wa kampuni au wa kibinafsi ambao unaficha eneo lako unaweza kusababisha gharama kuwa tofauti na zile zilizoonyeshwa za eneo lako halisi. Baadhi ya shughuli zinaweza kuhitaji kubadilishwa kwa sarafu za kigeni au kuchakatwa katika nchi nyingine kutegemea eneo lako. Huenda benki yako ikakulipisha ada ya ziada kwa huduma hizo wakati unapotumia kadi ya malipo au mkopo. Tafadhali wasiliana na benki yako kwa maelezo zaidi.
 • b. Akaunti yako ya Utozaji. Ili ulipie gharama ya Huduma, utaulizwa utoe mbinu ya malipo unapojiandikisha kwenye Huduma hiyo. Unaweza kufikia na kubadilisha maelezo yako ya akaunti ya utozaji na mbinu ya malipo kwenye Tovuti ya kusimamia akaunti ya Microsoft na kwa akaunti yako ya utozaji ya Skype kwa kuingia kwenye kituo cha akaunti yako kilicho https://skype.com/go/myaccount. Licha ya hayo, unakubali kuruhusu Microsoft kutumia maelezo yoyote yaliyosasishwa kuhusiana na mbinu yako uliyochagua ya malipo iliyotolewa na bengi yako au mtandao husika wa malipo. Unakubali kusasisha akaunti yako na maelezo mengine mara moja, ikiwa ni pamoja na anwani yako ya barua pepe na maelezo ya mbinu za malipo, ili tuweze kukamilisha shughuli zako na kuwasiliana na wewe ikihitajika kuhusiana na shughuli zako. Mabadiliko yaliyofanywa kwenye akaunti yako ya utozaji hayataathiri gharama tunazowasilisha kwenye akaunti yako ya bili kabla tuweze kuchukua hatua kuhusu mabadiliko yako ya akaunti yako ya bili.
 • c. Utozaji. Kwa kuipa Microsoft mbinu ya malipo, (i) unawakilisha kwamba umeidhinishwa kutumia mbinu ya malipo ambayo umetoa na kwamba maelezo yoyote ya malipo unayotoa ni ya kweli na sahihi; (ii) unaidhinisha Microsoft kukulipisha kwa Huduma au maudhui yanayopatikana kwa kutumia mbinu yako ya malipo; na (iii) unaidhinisha Microsoft kukulipisha kwa kipengele chochote cha kulipia cha Huduma ambazo unachagua kujiandikisha au kutumia wakati Masharti haya yanatumika. Tunaweza kukutoza (a) mapema; (b) wakati wa ununuzi; (c) muda mfupi baada ya ununuzi; au (d) kwa kurudia kwa Huduma za usajili. Pia, tunaweza kukulipisha hadi kiwango ulichoidhinisha, na tutakuarifu mapema kuhusu mabadiliko yoyote katika kiwango kinacholipishwa cha Huduma zinazoendelea za usajili. Huenda tukakutoza wakati mmoja kwa zaidi ya kipindi chako kimoja cha utozaji kwa viwango ambavyo havikuchakatwa awali.
 • d. Malipo Yanayojirudia. Wakati unaponunua Huduma kwa msingi wa usajili (k.m., kila mwezi, kila miezi 3 au kila mwaka), unakiri na kukubali kwamba unaidhinisha malipo kujirudia, na malipo yatalipwa kwa Microsoft kwa mbinu uliyochagua katika muda wa kujirudia uliokubaliana nao, hadi usajili wa Huduma hiyo ukatishwe na wewe au na Microsoft. Kwa kuidhinisha malipo yanayojirudia, unaidhinisha Microsoft kuchakata malipo hayo kwa njia ya malipo ya kielektroniki au uhamishaji wa fedha, au rasimu za kielektroniki kutoka kwa akaunti yako iliyoteuliwa (Taasisi Otomati ya Kifedha au malipo kama hayo), au kama malipo kwa akaunti yako iliyoteuliwa (kadi ya mkopo au malipo sawia) (kwa pamoja, Malipo ya Kielektroniki"). Ada za usajili kwa jumla hutozwa mapema kwa kipindi husika cha usajili. Ikiwa malipo yoyote yamerejeshwa au kutokulipwa au ikiwa kadi yoyote ya mkopo au shughuli kama hiyo imekataliwa, Microsoft au watoa huduma wake wana haki ya kukusanya kipengee chochote husika cha kurejeshwa, ada ya kukataliwa au ya fedha kutotosha na kuchakata malipo yoyote kama hayo kama Malipo ya Kielektroniki.
 • e. Ubadilishaji otomatiki. Ikiwa otomatiki imeruhusiwa chini ya sheria husika, unaweza kuchagua Huduma ibadilishe kiotomatiki mwisho wa kipindi kilichowekwa cha huduma. Tutakukumbusha kwa barua pepe, au kwa njia nyingine inayofaa, kabla ya Huduma zozote kubadilishwa kwa muhula mpya, na tutakuarifu kuhusu mabadiliko yoyote kulingana na sehemu ya 9(k). Tunapokukumbusha kwamba umechagua Huduma kubadilishwa kiotomatiki, tunaweza kubadilisha Huduma zako kiotomatiki mwishoni mwa kipindi cha sasa cha huduma na kukutoza ada ya sasa kwa muhula huo mpya, isipokuwa iwe umechagua kukatisha Huduma kama ilivyofafanuliwa hapa chini. Tutakukumbusha pia tutatoza mbinu yako uliyochagua ya malipo ya ubadilishaji Huduma, iwe ilikuwa kwenye faili wakati wa tarehe ya kubadilisha au ilitolewa baadaye. Tutakupa pia maagizo kuhusu jinsi unavyoweza kukatisha Huduma. Lazima ukatishe Huduma kabla ya tarehe ya kubadilisha ili uepuke kutozwa ubadilishaji.
 • f. Taarifa ya Mtandaoni na Hitilafu. Microsoft itakupa taarifa ya bili ya mtandaoni kwenye tovuti ya ya kusimamia akaunti ya Microsoft, ambapo unaweza kutazama na kuchapisha taarifa yako. Kwa Skype, unaweza kufikia taarifa yako ya mtandaoni kwa kujiandikisha kwenye akaunti yako kwenye www.skype.com. Hii ndiyo taarifa ya bili tu ambayo tunatoa. Tukifanya makosa kwenye bili yako, lazima utueleze ndani ya siku 90 baada ya hitilafu kutokea mara kwa kwanza kwenye bili yako. Kisha tutachunguza kwa haraka gharama hiyo. Ukikosa kutueleza ndani ya wakati huo, unatuondoa kwenye dhamana na madai yote ya hasara inayotokana na hitilafu na hatutahitaji kusahihisha hitilafu au kutoa fidia, isipokuwa iwe inahitajika kisheria. Ikiwa Microsoft imetambua hitilafu ya bili, tutasahihisha hitilafu hiyo ndani ya siku 90. Sera hii haiathiri haki zozote za kisheria ambazo zinaweza kutumika.
 • g. Sera ya Fidia. Isipokuwa iwe imetolewa na sheria au toleo maalum la Huduma, ununuzi wote ni wa mwisho na huwezi kurejeshwa. Ikiwa unaamini kwamba Microsoft imekulipisha kimakosa, lazima uwasiliane na sisi ndani ya siku 90 kuhusu malipo hayo. Hakuna kurejeshewa fedha kutakaotolewa kwa gharama zozote zaidi ya siku 90, isipokuwa iwe inahitajika kisheria. Tunahifadhi haki ya kutoa fidia au mikopo kwa uamuzi wetu. Tukitoa fidia au mkopo, hatuwajibiki kutoa fidia sawa au sawia baadaye. Fidia hii haiathiri haki zozote za kisheria ambazo zinaweza kutumika. Kwa maelezo zaidi ya fidia, tafadhali tembelea mada ya usaidizi. Ikiwa unaishi Taiwani, tafadhali kumbuka kwamba kulingana na Sheria ya Kuwalinda Wateja wa Taiwani na sheria zake husika, ununuzi wote unaohusiana na maudhui ya kidijitali yanayotolewa kupitia fomu zisizogusika na/au huduma za mtandaoni ni kamili na haziwezi kufidiwa wakati maudhui au huduma kama hizo zimetolewa mtandaoni. Huna haki ya kudai muda wowote wa majaribio au fidia yoyote.
 • h. Kukatisha Huduma. Unaweza kukatisha Huduma wakati wowote na au bila sababu yoyote. Ili kusitisha Huduma na kuomba fidia, ikiwa unastahili kufidiwa, tembelea tovuti ya kusimamia akaunti ya Microsoft. Kwa Skype, tafadhali kamilisha Fomu ya Kutoa kwa kutumia maelezo yaliyotolewa hapa. Unapaswa kurejelea toleo linalofafanua Huduma kama (i) unaweza kupokea fidia wakati wa ukatishaji; (ii) unaweza kuwajibika kulipia gharama ya ukatishaji; (iii) unaweza kuwajibika kulipia gharama zote zilizofanywa kwenye akaunti yako ya utozaji kwa huduma kabla ya tarehe ya ukatishaji; na (iv) unaweza kupoteza ufikiaji na matumizi ya akaunti yako unapokatisha Huduma; au, ikiwa unaishi Taiwani, (v) unaweza kupokea fidia ya kiwango ambacho ni sawa na ada uliyolipa isiyotumiwa kwa Huduma ikihesabiwa wakati wa ukatishaji. Tutachakata Data yako kama ilivyofafanuliwa hapa juu katika sehemu ya 4. Ukikatisha, ufikiaji wako wa Huduma huisha mwisho wa kipindi chako cha sasa cha Huduma au, tukitoza akaunti yako mara kwa mara, mwisho wa kipindi ambacho ulikatisha.
 • i. Matoleo ya Muda wa Majaribio. Ikiwa unahusika katika toleo lolote la muda wa majaribio, lazima ukatishe Huduma hizo za majaribio kabla ya mwisho wa kipindi cha jaribio ili uepuke kupata gharama mpya, isipokuwa tukuarifu kivingine. Ukikosa kukatisha Huduma za majaribio kabla ya mwisho wa kipindi cha jaribio, huenda tukakulipisha kwa Huduma hizo.
 • j. Ofa za Matangazo. Mara kwa mara, huenda Microsoft ikatoa Huduma bila malipo kwa kipindi cha majaribio. Microsoft inahifadhi haki ya kukulipisha kwa Huduma kama hizo (kwa kiwango cha kawaida) kama Microsoft itabainisha (kwa uamuzi wake) kwamba unatumia vibaya masharti ya toleo.
 • k. Mabadiliko ya Bei. Tunaweza kubadilisha bei ya Huduma wakati wowote na ikiwa una ununuzi unaojirudia, tutakuarifu kwa barua pepe, au kwa njia nyingine inayofaa, angalau siku 15 kabla ya mabadiliko ya bei. Ikiwa hukubaliani na mabadiliko ya bei, lazima ukatishe na ukome kutumia Huduma kabla ya mabadiliko ya bei kuanza kutumika. Ikiwa kuna muda na bei iliyowekwa ya toleo la Huduma yako, bei hiyo itaendelea kutumika kwa muda huo uliowekwa.
 • l. Malipo Kwako. Ikiwa unatudai malipo, basi unakubali kutupa kwa wakati unaofaa na kwa usahihi maelezo yoyote tunayohitaji ili kukupa malipo hayo. Unawajibika kwa ushuru na gharama zozote unazoweza kupata kama matokeo ya malipo haya kwako. Lazima pia ufuate hali zozote tulizoweka kwenye haki yako ya malipo yoyote. Ikiwa umepokea malipo kimakosa, huenda tukabatilisha au tukahitaji urejeshe malipo hayo. Unakubali kushirikiana nasi katika juhudi zetu za kufanya hivi. Tunaweza pia kupunguza malipo kwako bila ilani ili kurekebisha malipo yoyote ya ziada ya awali.
 • m. Kadi za Zawadi. Ukomboaji na matumizi ya kadi za zawadi (kando na kadi za zawadi za Skype) husimamiwa na Sheria na Mashari ya Kadi za Zawadi za Microsoft. Maelezo kuhusu kazi za zawadi za Skype yanapatikana kwenye Ukurasa wa Msaada wa Skype.
 • n. Mbinu ya Malipo ya Akaunti ya Benki. Unaweza kusajili akaunti inayostahiki ya benki kwa kutumia akaunti yako ya Microsoft ili kutumia kama mbinu ya malipo. Akaunti zinazostahiki za benki ni pamoja na akaunti zinazomilikiwa na taasisi ya kifedha inayoweza kupokea pesa moja kwa moja (k.m., taasisi ya kifedha iliyo Marekani ambayo inakubali taasisi otomati za kifedha ("ACH"), taasisi ya kifedha ya Ulaya ambayo inakubali Eneo la Malipo ya aina Moja ya Yuro ("SEPA") au "iDEAL" nchini Uholanzi). Masharti hukubaliwa wakati wa kuongeza akaunti yako ya benki kama mbinu ya malipo katika akaunti yako ya Microsoft (k.m. "udhamini" katika hali ya SEPA) hutumika pia. Unawakilisha na kuhakikisha kwamba akaunti yako iliyosajiliwa ya benki iko kwenye jina lako au umeidhinishwa kusajili na kutumia akaunti hii ya benki kama mbinu ya malipo. Kwa kusajili au kuteua akaunti ya benki yako kama mbinu yako ya malipo, unaidhinisha Microsoft (au wakala wake) kuanzisha malipo kwa kiasi cha jumla cha ununuzi wako au ada ya usajili (kulingana na masharti ya huduma yako ya usajili) kutoka kwa akaunti yako ya benki (na, ikihitajika, kuanzisha malipo kwa akaunti yako ya benki ili kusahihisha makosa, kutoa fidia au lengo kama hilo), na unaidhinisha taasisi ya kifedha ambayo inamiliki akaunti yako ya benki kupunguza malipo kama hayo au kukubali mikopo kama hiyo. Unaelewa kwamba idhini hii itaendelea kutumika kabisa hadi uondoe maelezo ya akaunti yako ya benki kutoka kwa akaunti yako ya Microsoft. Wasiliana na usaidizi kwa wateja kama ilivyoorodheshwa hapa juu katika sehemu ya 4(e) haraka iwezekanavyo ikiwa unaamini umetozwa kimakosa. Sheria zinazotumika katika nchi yako zinaweza pia kuzuia dhima yako ya miamala yoyote ya ulaghai, kimakosa, au isiyoidhinishwa kutoka kwa akaunti yako ya benki. Kwa kusajili au kuteua akaunti ya benki kama mbinu yako ya malipo, unakubali kwamba umesoma, kuelewa na kukubaliana na Masharti haya.
Maandishi kamili
Shirika linalotoa Mkataba, Chaguo la Kisheria, na Eneo la Kutatua MizozoShirika linalotoa Mkataba, Chaguo la Kisheria, na Eneo la Kutatua Mizozo10_11_contractingEntityChoiceOfLaw
Muhtasari

10. Shirika linalotoa Mkataba, Chaguo la Kisheria, na Eneo la Kutatua Mizozo. Kwa matumizi yako ya Huduma zenye chapa ya Skype zisizolipishwa na zinazolipishwa za watumiaji, unazofanya mkataba nazo, na marejeleo yote ya "Microsoft" katika Masharti haya humaanisha, Skype Communications S.à.r.l, 23 – 29 Rives de Clausen, L-2165 Luxembourg. Kwa Huduma zisizolipishwa au zinazolipishwa za watumiaji zenye chapa ya Skype, Sheria ya Lasembagi husimamia utafsiri wa Masharti haya na madai ya ukiukaji, haijalishi mgongano wa kanuni za kisheria. Sheria za mkoa au nchi unayoishi husimamia madai yale mengine yote (ikiwa ni pamoja na kuwalinda wateja, ushindani usio wa haki, na madai ya kosa la daawa). Ukikubali Masharti haya kwa kufungua akaunti ya Skype au kutumia Skype, wewe na sisi tunakubali kwa mamlaka ya kipekee na mahali pa mahakama ya Lasembagi kwa mizozo yote inayoibuka au inayohusiana na Masharti haya au Huduma za watumiaji zenye chapa ya Skype. Kwa Huduma nyingine zote, ikiwa ulikubali Masharti haya kwa kufungua akaunti ya Microsoft au kwa kutumia Huduma nyingine yoyote na shirika la mkataba, sheria husika, na eneo la kutatua mizozo linatokea hapa chini:

 • a. Kanada. Ikiwa unaishi (au, ikiwa ni biashara, makao yako makuu ya biashara) yako nchini Kanada, una mkataba na Microsoft Corporation, One Microsoft Way, Redmond, WA 98052, U.S.A. Sheria za mkoa unaoishi (au, ikiwa ni biashara, makao yako makuu ya biashara) zitasimamia utafsiri wa Masharti Haya, ikiwa ni pamoja na ukiukaji wake, na madai mengine yote (ikiwa ni pamoja na kuwalinda watumiaji, ushindani usio wa haki, na madai ya kosa la daawa), haijalishi mgongano wa kanuni za sheria. Wewe na sisi tunakubali kwa mamlaka ya kipekee na mahali pa mahakama nchini Ontario kwa mizozo yote inayoibuka au inayohusiana na Masharti haya au Huduma.
 • b. Marekani ya Kaskazini au Kusini nje ya Marekani na Kanada. Ikiwa unaishi (au, ikiwa ni biashara, makao yako makuu ya biashara) yako Marekani ya Kaskazini au ya Kusini nje ya Marekani na Kanada, una mkataba na Microsoft Corporation, One Microsoft Way, Redmond, WA 98052, U.S.A. Sheria za Jimbo la Washington zitasimamia utafsiri wa Masharti Haya na ukiukaji wake, haijalishi chaguo la kanuni za sheria. Sheria za nchi ambayo tunaelekeza Huduma zetu husimamia madai yale mengine yote (ikiwa ni pamoja na kuwalinda wateja, ushindani usio wa haki, na madai ya kosa la daawa).
 • c. Mashariki ya Kati au Afrika. Ikiwa unaishi (au, ikiwa ni biashara, makao yako makuu ya biashara) yako Mashariki ya Kati au Afrika, na unatumia sehemu zisizolipishwa za Huduma (kama vile Bing na MSN), una mkataba na Microsoft Corporation, One Microsoft Way, Redmond, WA 98052, U.S.A. Ikiwa ulilipa kutumia sehemu ya Huduma, una mkataba na Microsoft Ireland Operations Limited, One Microsoft Place, South County Business Park, Leopardstown, Dublin 18, Ireland. Kwa Huduma zisizolipishwa na zinazolipishwa, sheria za Ayalandi husimamia utafsiri wa Masharti haya na madai ya ukiukaji, haijalishi mgongano wa kanuni za sheria. Sheria za nchi ambayo tunaelekeza Huduma zetu husimamia madai yale mengine yote (ikiwa ni pamoja na kuwalinda wateja, ushindani usio wa haki, na madai ya kosa la daawa). Wewe na sisi tunakubali kwa mamlaka ya kipekee na mahali pa mahakama ya Ayalandi kwa mizozo yote inayoibuka au inayohusiana na Masharti haya au Huduma.
 • d. Asia au Pasifiki Kusini, isipokuwa nchi yako iwe imetajwa hapa chini. Ikiwa unaishi (au, kama ni biashara, eneo lako msingi la biashara ni) Asia (isipokuwa Uchina, Japani, Jamhuri ya Korea, au Taiwani) au Pasifiki ya Kusini, na unatumia sehemu za bila malipo za Huduma (kama vile Bing na MSN), una mkataba na Microsoft Corporation, One Microsoft Way, Redmond, WA 98052, U.S.A. Ikiwa ulilipa kutumia sehemu ya Huduma, au unatumia huduma ya Outlook.com bila malipo nchini Singapoo au Hong Kong, una mkataba na Microsoft Regional Sales Corp., shirika lililopangwa chini ya sheria za Jimbo la Nevada, Marekani, na lina matawi nchini Singapoo na Hong Kong, ikiwa na eneo lake msingi la biashara katika 438B Alexandra Road, #04-09/12, Block B, Alexandra Technopark, Singapore, 119968; bora ikiwa unaishi (au, kama ni biashara, eneo lako msingi la biashara ni) Australia, una mkataba na Microsoft Pty Ltd, 1 Epping Road, North Ryde, NSW 2113, Australia na ikiwa unaishi katika (au, ikiwa ni biashara, eneo lako msingi la biashara liko) Nyuzilandi, una mkataba na Microsoft New Zealand Limited, Level 5, 22 Viaduct Harbour Avenue, PO Box 8070 Symonds Street, Auckland, 1150 New Zealand. Kwa Huduma zisizolipishwa au zinazolipishwa, Sheria ya jimbo la Washington husimamia utafsiri wa Masharti haya na madai ya ukiukaji, haijalishi mgongano wa kanuni za kisheria. Sheria za nchi ambayo tunaelekeza Huduma zetu husimamia madai yale mengine yote (ikiwa ni pamoja na kuwalinda wateja, ushindani usio wa haki, na madai ya kosa la daawa). Mzozo wowote unaotokana na au unaohusiana na Masharti au Huduma kando na Skype, ikiwa ni pamoja na swali lolote kuhusiana na kuwepo, uhalali au usitishaji wake, utaelekezwa na mwishowe kutatuliwa na usuluhishi nchini Singapoo kulingana na Kanuni za Usuluhishaji za Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishaji cha Singapoo (SIAC), ambazo sheria zake huchukuliwa kuwa zimejumuishwa kwa kurejelea kifungu hiki. Baraza hili litakuwa na msuluhishi mmoja atakayeteuliwa na Rais wa SIAC. Lugha ya usuluhishaji itakuwa Kiingereza. Uamuzi wa msluhushi utakuwa wa mwisho, unaofunga, na usioweza kupingwa, na unaweza kutumiwa kama msingi wa uamuzi katika nchi au eno lolote.
 • e. Japani. Ikiwa unaishi (au, ikiwa ni biashara, makao yako makuu ya biashara) yako nchini Japani, na unatumia sehemu zisizolipishwa za Huduma (kama vile Bing na MSN), una mkataba na Microsoft Corporation, One Microsoft Way, Redmond, WA 98052, U.S.A. Ikiwa ulilipa kutumia sehemu ya Huduma, una mkataba na Microsoft Japan Co., Ltd (MSKK), Shinagawa Grand Central Tower, 2-16-3 Konan Minato-ku, Tokyo 108-0075. Kwa Huduma zisizolipishwa na zinazolipishwa, sheria za Japani husimamia Masharti haya na masuala yoyote yanayoibuka au yanayohusiana nazo au Huduma. Wewe na sisi tunakubali kwa mamlaka halisi ya kipekee na mahali pa mahakama ya Mahakama ya Mkoa wa Tokyo kwa mizozo yote inayoibuka au inayohusiana na Masharti haya au Huduma.
 • f. Jamhuri ya Korea. Ikiwa unaishi (au, ikiwa ni biashara, makao yako makuu ya biashara) yako katika Jamhuri ya Korea, na unatumia sehemu zisizolipishwa za Huduma (kama vile Bing na MSN), una mkataba na Microsoft Corporation, One Microsoft Way, Redmond, WA 98052, U.S.A. Ikiwa ulilipa kutumia sehemu ya Huduma, una mkataba na Microsoft Korea, Inc., 11th Floor, Tower A, K-Twin Tower, Jongro 1 gil 50, Jongro-gu, Seoul, Republic of Korea, 110-150. Kwa Huduma zisizolipishwa na zinazolipishwa, sheria za Jamhuri ya Korea husimamia Masharti haya na masuala yoyote yanayoibuka au yanayohusiana nazo au Huduma. Wewe na sisi tunakubali kwa mamlaka halisi ya kipekee na mahali pa mahakama ya Mahakama ya Mkoa wa Kati wa Seoul kwa mizozo yote inayoibuka au inayohusiana na Masharti haya au Huduma.
 • g. Taiwani. Ikiwa unaishi (au, ikiwa ni biashara, makao yako makuu ya biashara) yako nchini Taiwani, na unatumia sehemu zisizolipishwa za Huduma (kama vile Bing na MSN), una mkataba na Microsoft Corporation, One Microsoft Way, Redmond, WA 98052, U.S.A. Ikiwa ulilipa kutumia sehemu ya Huduma, una mkataba na Microsoft Taiwan Corp., 18F, No. 68, Sec. 5, Zhongxiao E. Rd., Xinyi District, Taipei 11065, Taiwan. Kwa Huduma zisizolipishwa na zinazolipishwa, sheria za Taiwani husimamia Masharti haya na masuala yoyote yanayoibuka au yanayohusiana nazo au Huduma. Kwa maelezo zaidi yanayohusiana na Microsoft Taiwan Corp., tafadhali angalia tovuti iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Uchumi R.O.C.. Wewe na sisi tunateua Mahakama ya Wilaya ya Taipei kuwa mahakama ya kwanza yenye utawala kwa mizozo yote inayoibuka au inayohusiana na Masharti haya au Huduma, kwa umbali wa juu unaokubaliwa na sheria za Taiwani.

Huenda sheria za watumiaji za eneo lako zikahitaji baadhi ya sheria za eneo lako kusimamia au kukupa haki ya kutatua mizozo katika mdahalao mwingine licha ya Masharti haya. Ikiwa ni hivyo, chaguo la sheria na matoleo ya mdahalo katika sehemu ya 10 hutumika kulingana na jinsi sheria za watumiaji za eneo lako zinaruhusu.

Maandishi kamili
WarantiWaranti12_Warranties
Muhtasari

11. Waranti.

 • a. MICROSOFT, NA MAKAMPUNI YETU TANZU, WAUZAJI, WASAMBAZAJI, NA WACHUUZI, HAWATOA WARANTI ZOZOTE, ZA MOJA KWA MOJA AU ZA KUDOKEZWA, HAKIKISHO AU MASHARTI KUHUSIANA NA MATUMIZI YAKO YA HUDUMA. UNAFAHAMU KWAMBA MATUMIZI YA HUDUMA HIZO NI JUU YAO NA KWAMBA TUNATOA HUDUMA KWA MSINGI WA "JINSI ILIVYO" "NA DOSARI ZOTE" NA "KAMA INAVYOPATIKANA." MICROSOFT HAIHAKIKISHI USAHIHI AU UMILELE WA HUDUMA. HUENDA UKAWA NA HAKI NYINGINE CHINI YA SHERIA ZA ENEO LAKO. HAKUNA CHOCHOTE KATIKA MASHARTI HAYA YALIYOKUSUDIWA KUATHIRI HAKI ZAKO, IKIWA KIPO. UNAKUBALI KWAMBA MIFUMO YA KOMPYUTA NA MAWASILIANO HAYAKOSI DOSARI NA HUENDA KUKAWA NA NYAKATI HAZITAFANYA KAZI. HATUHAKIKISHI HUDUMA HAZITATATIZWA, ZITAKUWA KWA WAKATI UNAOFAA, SALAMA, AU HAZITAKOSA HITILAFU AU KWAMBA MAUDHUI YATAWEZA KUPOTEA, WALA HATUHAKIKISHI MUUNGANISHO AU UPITISHAJI WOWOTE KUTOKA KWENYE MITANDAO YA KOMPYUTA.
 • b. KWA UMBALI UNAORUHUSIWA CHINI YA SHERIA YA ENEO LAKO, HATUJUMUISHI WARANTI ZOZOTE ZA KUNUKULIWA, IKIWA NI PAMOJA NA UUZAJI, UBORA WA KURITHIKA, KUFAA LENGO FULANI, JUHUDI ZA USTADI, NA KUTOKIUKA.
 • c. Kwa watumiaji nchini Australia: Bidhaa zetu huja na hakikisho ambazo haziwezi kutengwa chini ya Sheria ya Watumiaji wa Australia. Una haki ya kubadilishiwa au kurejeshewa fedha kwa tatizo kubwa na fidia kwa hasara au uharibifu wowote unaoweza kuonekana. Una haki pia ya bidhaa kukarabatiwa au kubadilishwa ikiwa bidhaa haitakuwa na ubora unaokubalika na shida hiyo haitasababisha hasara kubwa.
 • d. Kwa watumiaji wanaoishi nchini Nyuzilandi, huenda ukawa na haki za kisheria chini ya Sheria ya Hakikisho za Watumiaji wa Nyuzilandi, na hakuna chochote katika Masharti haya yanakusudiwa kuathiri haki hizo.
Maandishi kamili
Kikomo cha DhimaKikomo cha Dhima13_limitationOfLiability
Muhtasari

12. Kikomo cha Dhima.

 • a. Ikiwa una msingi wowote wa kurejeshewa hasara (ikiwa ni pamoja na ukiukaji wa Masharti haya), kwa kadiri inayoruhusiwa na sheria husika, unakubali kwamba suluhisho lako la kipekee ni kurejesha, kutoka kwa Microsoft au makampuni yake tanzu, wauzaji, wasambazaji, watoaji Wengine wa Huduma na Programu, na wachuuzi, hasara ya moja kwa moja ilio sawa na kiwango cha ada yako ya Huduma kwa mwezi ambao upotezaji au ukiukaji ulifanyika (au hadi USD$10.00 ikiwa Huduma hazilipishwi).
 • b. Kwa kiasi kinachoruhusiwa na sheria husika, huwezi kufidiwa (i) hasara au uharibifu wowote unaotokana na; (ii) hasara ya faida halisi au zinazotarajiwa (iwe za moja kwa moja au zisizo za moja kwa moja); (iii) hasara halisi au inayotarajiwa ya mapato (iwe za moja kwa moja au zisizo za moja kwa moja); (iv) kukosa kandarasi au biashara au hasara au uharibifu wowote unaotokana na matumizi yako ya Huduma katika wadhifa usio wa kibinafsi; (v) hasara au uharibifu maalum, usio wa moja kwa moja, wa bahati mbaya au wa nidhamu; na (vi) kwa umbali unaoruhusiwa na sheria, hasara au uharibifu wa moja kwa moja unaozidi kikomo kilichobainishwa katika sehemu ya 12(a) hapo juu. Vizuizi na vitengwaji hivi hutumika ikiwa suluhisho hili halikufidii kabisa kwa hasara au matatizo yoyote ya lengo lake kuu au ikiwa tulifahamu au tungefahamu kuhusu uwezekano wa hasara. Kwa umbali unaoruhusiwa na sheria, vizuizi na vintengwaji hivi hutumika kwa kitu chochote au madai yoyote yanayohusiana na Masharti haya, Huduma, au programu inayohusiana na Huduma.
 • c. Microsoft haiwajibiki kwa tatizo lolote la kutekeleza au kuchelewa kutekeleza majukumu yake chini ya Masharti haya kwa umbali kwamba tatizo au kuchelewa huko kunasababishwa na hali ambazo haziwezi kudhibitiwa na Microsoft (kama vile mizozo ya wafanyakazi, vitendo vya Mungu, shughuli za kivita au ugaidi, uharibifu kwa nia mbaya, ajali au kuafikiana na sheria zozote husika au agizo la serikali). Microsoft itajitahidi kupunguza athari za yoyote kati ya matukio haya na kutekeleza majukumu ambayo hayajaathiriwa.
Maandishi kamili
Masharti Maalum ya HudumaMasharti Maalum ya Huduma14_service-SpecificTerms
Muhtasari

13. Masharti Maalum ya Huduma. Masharti kabla na baada ya sehemu 13 hutumika kwa ujumla kwa Huduma zote. Sehemu hii ina masharti maalum ya huduma ambayo ni nyongeza ya masharti ya jumla. Masharti haya maalum ya huduma yanasimamia ikiwa kuna migongano yoyote na masharti ya jumla.

Maandishi kamili
Michezo na Programu za Xbox Live na Microsoft StudiosMichezo na Programu za Xbox Live na Microsoft Studios14a_XboxLive
Muhtasari
 • a. Michezo na Programu za Xbox Live na Microsoft Studios.
  • i. Matumizi ya Kibinafsi Yasio ya Kibiashara. Xbox Live, Michezo ya Windows Live na michezo ya Microsoft Studios, programu, huduma na maudhui yanayotolewa na Microsoft (kwa pamoja, "Huduma za Xbox") ni za matumizi ya kibinafsi na yasiyo ya kibiashara tu.
  • ii. Huduma za Xbox. Unapojiandikisha kwa Huduma za Xbox Live na/au kupokea Huduma za Xbox, maelezo kuhusu unavyocheza michezo, shughuli na matumizi ya michezo na Huduma za Xbox zitafuatiliwa na kushirikiwa na wasanidi programu wengine husika wa michezo ili Microsoft na wasanidi programu wengine wa michezo kuendesha michezo yao na kuwasilisha Huduma za Xbox. Ukichagua kuunganisha akaunti yako ya Huduma za Microsoft Xbox na akaunti yako kwenye huduma isiyo ya Microsoft (kwa mfano, mchapishaji wa michezo asiye wa Microsoft wa Programu na Huduma za wahusika wengine), unakubali kwamba: (a) Microsoft inaweza kushiriki maelezo machache ya akaunti (ikiwa ni pamoja na lebo ya mchezaji, alama za mchezaji, alama za mchezo, historia ya mchezo, na orodha ya marafiki), na mhusika huyo asiye wa Microsoft kama ilivyoelezewa katika Taarifa ya Faragha ya Microsoft, na (b) ikiwa inaruhusiwa na mipangilio yako ya faragha ya Xbox, mhusika ambaye si wa Microsoft anaweza pia kufikia Maudhui Yako kutoka kwa mawasiliano ya ndani ya mchezo unapoingia katika akaunti yako kwa kutumia mhusika huyo asiye wa Microsoft. Pia, ikiruhusiwa na mipangilio yako ya faragha ya Xbox, Microsoft inaweza kuchapisha jina lako, lebo ya mchezaji, picha ya mchezaji, mwito, uhuishaji, klipu za michezo na michezo ambayo umecheza katika mawasiliano na watu unaowaruhusu.
  • iii. Maudhui Yako. Kama sehemu ya ujenzi wa jumuia ya Huduma za Xbox, unaipa Microsoft, makampuni yake tanzu, na watoa leseni wengine wadogo haki isiyolipishwa na ya duniani kote, ya kutumia, kurekebisha, kuzalisha upya, kusambaza, kutangaza, kushiriki na kuonyesha Maudhui Yako au jina lako, lebo ya mchezaji, kauli, au uhuisho ambao ulichapisha kwa Huduma zozote za Xbox.
  • iv. Wasimamizi wa Mchezo. Huenda baadhi ya michezo ikatumia wasimamizi na wapangishaji wa mchezo. Wasimamizi na wapangishi wa mchezo sio wanenaji waliodhinishwa wa Microsoft. Maoni yao hayaangazii yale ya Microsoft.
  • v. Watoto kwenye Xbox. Ikiwa wewe ni mtoto unayetumia Xbox Live, mzazi au mlezi wako huenda ana udhibiti wa vipengee vingi vya akaunti yako na huenda akapokea ripoti kuhusu matumizi yako ya Xbox Live.
  • vi. Sarafu ya Mchezo au Bidhaa Pepe. Huenda Huduma zikajumuisha, sarafu pepe ya mchezo (kama vile dhahabu, sarafu au pointi) ambazo zinaweza kununuliwa kutoka kwa Microsoft kwa kutumia pesa halisi ikiwa umefikia umri wa "wengi" unakoishi. Huenda Huduma zikajumuisha pia vipengee au bidhaa pepe vya kidijitali ambazo zinaweza kununuliwa kutoka kwa Microsoft kwa kutumia pesa halisi au kwa kutumia sarafu ya mchezo. Huenda sarafu ya mchezo na bidhaa pepe zisiweze kukombolewa kwa pesa, bidhaa au vipengele vingine halisi vyenye thamani ya pesa kutoka kwa Microsoft au mhusika mwingine yeyote. Kando na leseni yenye kikomo, ya kibinafsi, isiyoweza kubatilishwa, isiyoweza kuhamishwa, isiyoweza kutolewa leseni nyingine ya kutumia sarafu ya mchezo na bidhaa pepe katika Huduma tu, huna haki ya sarafu kama hiyo ya mchezo au bidhaa pepe zinazotokea au kuanzishwa katika Huduma, au sifa nyingine zozote zinazohusishwa na matumizi ya Huduma au kuhifadhiwa kwenye Huduma. Huenda wakati mwingine Microsoft ikasimamia, kudhibiti, kurekebisha na/au kuondoa sarafu ya mchezo na/au bidhaa pepe kulingana na uamuzi wake.
  • vii. Visasisho vya Programu. Kwa kifaa chochote ambacho kinaweza kuunganishwa kwenye Huduma za Xbox, tunaweza kukagua toleo lako la programu ya kiweko cha Xbox au programu ya Xbox kiotomatiki na kupakua visasisho vya kiweko cha Xbox au programu ya Xbox au mabadiliko ya usanidi, ikiwa ni pamoja na zile ambazo zinakuzuia kufikia Huduma za Xbox, kutumia michezo au programu zisizoidhinishwa za Xbox, au kutumia vifaa vya ziada vya maunzi ambavyo havijaidhinishwa na kiweko cha Xbox.
  • viii. Muda wa lebo ya mchezaji kuisha. Lazima uingie katika Huduma za Xbox angalau mara moja katika kipindi cha miaka mitano, la sivyo unaweza kupoteza idhini yako ya kufikia lebo ya mchezaji inayohusishwa na akaunti yako na lebo hiyo ya mchezaji ikapewa watu wengine waitumie.
  • ix. Arena. Arena ni Huduma ya Xbox Service ambayo Microsoft au wahusika wengine wanaweza kukupa uwezo wa kushiriki katika kuunda mashindano ya michezo ya video, wakati mwingine ili kupata zawadi ("Mashindano"). Matumizi yako ya Arena yanategemea Masharti haya, na huenda yakakuhitaji ukubali masharti, sheria na kanuni za ziada za Mashindano zinazohitajika na Wapangaji wa mashindano wakati unapojiandikisha ("Masharti ya Mashindano"). Kanuni za kustahiki zinaweza kutumika, na zinaweza kutofautiana kimaeneo. Mashindano si halali katika maeneo yaliyokatazwa au kuwekewa vikwazo na sheria. Ukiukaji wa Masharti haya (ikiwa ni pamoja na Kanuni ya Maadili Mema) au Masharti ya Mashindano unaweza kusababisha kuadhibiwa au kuondolewa kwenye Mashindano. Ukiunda Mashindano, huenda usihitaji Sheria zozote za Mashindano ambazo Microsoft (kwa uamuzi wake) inaonelea hazilingani na Masharti haya. Microsoft inahifadhi haki ya kukatisha Mashindano yoyote wakati wowote.
  • x. Programu ya Kulaghai na Kushindilia. Kwa kifaa chochote ambacho kinaweza kuunganishwa kwenye Huduma za Xbox, tunaweza kukagua kifaa chako kwa maunzi au programu isiyoidhinishwa ambayo huwezesha ulaghai na ushindiliaji kwa kukiuka Kanuni ya Maadili Mema ya Masharti haya, na kupakua visasisho vya programu vya Xbox au mabadiliko ya usanidi, ikiwa ni pamoja na zile ambazo zinakuzuia kufikia Huduma za Xbox, au dhidi ya kutumia maunzi au programu isiyoidhinishwa ambayo huwezesha kulaghai au ushindiliaji.
  • xi. Mixer.
   • 1. Akaunti za Mixer na Akaunti za Microsoft. Ukiwa unatimia Huduma ya Mixer pamoja na Akaunti ya Mixer, basi matumizi yako yanasimamiwa na Masharti ya Huduma ya Mixer yanayopatikana kwenye https://mixer.com/about/tos. Ikiwa unatumia Huduma ya Mixer pamoja na akaunti ya Microsoft, basi matumizi yako yanasimamiwa pia na Masharti haya. Masharti haya yanatumika mahali kuna mzozo.
   • 2. Maudhui Yako kwenye Mixer. "Maudhui Yako kwenye Mixer" humaanisha maudhui yote ambayo wewe, au mtu mwingine kwa niaba yako, aliunda kwenye Huduma ya Mixer, ikiwa ni pamoja lakini haijakomea kwa mitiririsho ya moja kwa moja na iliyorekodiwa (na maudhui yoyote, kama vile maudhui ya sauti na maonyesho, ambayo yanayo); majina ya chapa, alama za biashara, alama za huduma, majina ya bishara, nembo, au indicia ya asili; maoni yako, ikonihisia, na shughuli katika vituo vya Mixer (ikiwa ni pamoja na maudhui yanayozalishwa na bot); na metadata zote zinazohusiana Mtu yeyote, ikiwa ni pamoja na Microsoft na watumiaji, wanaweza kuona, kutumia kupangisha, kuzalisha upya, kurekebisha, kusambaza, kuchapisha, kutekeleza na kuonyesha hadharani na kidijitali, kutafsiri, kuchukua, na kutumia Maudhui Yako kwenye Mixer, kwa njia, umbizo, midia, vituo vyovyote vile vinavyojulikana sasa au kutengenezwa baadaye.
   • 3. Kanuni ya Maadili Mema Inayotumika kwenye Mixer. Bofya hapa kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi Kanuni ya Maadili Mema ya Microsoft inatumika kwenye Mixer.
   • 4. Kutumia Huduma ya Mixer.
    • a. Umri wa Chini. Kwa kutumia Huduma ya Mixer, unamaanisha kwamba umefikia angalau miaka 13 na, ukiwa uko chini ya umri wa wengi mahali unakoishi, matumizi yako yanasimamiwa na mzazi au mlezi wa kisheria.
    • b. Matumizi Yanayojulikana na Yasiyojulikana. Unaweza kutumia Mixer bila kujulikana kama unataka kuona maudhui pekee. Kama sivyo, unahitaji kufungua akaunti, kuingia, na utatambuliwa kwa watumiaji wengine na jina lako la Mixer.
    • c. Akaunti za Matumizi Yasiyojulikana. Unaweza kufungua akaunti ya Microsoft na/au akaunti ya Mixer kwa matumizi yasiyojulikana ya Huduma ya Mixer. Unaweza kufungua akaunti ya Mixer kwa kujiandikisha mtandaoni. Lazima utumie akaunti yako ya Mixer ili iendelee kutumika. Lazini uingie kwenye Huduma ya Mixer angalau mara moja katika kipindi cha miaka 5 ili kudumisha jina lako la Mixer linakohusishwa na akaunti yako ya Microsoft.
   • 5. Arifa za Huduma. Wakati kuna kitu muhimu tunachotaka kukueleza kuhusu Huduma ya Mixer, tutakutumia arifa za Huduma kwa barua pepe inayohusishwa na akaunti yako ya Mixer na/au Microsoft.
   • 6. Usaidizi. Usaidizi kwa wateja kwa Huduma ya Mixer unapatikana kwenye mixer.com/contact.
Maandishi kamili
DukaDuka14b_Store
Muhtasari
 • b. Duka. "Duka" hurejelea Huduma ambayo hukuwezesha kuvinjari, kupakua, kununua, na kukadiria na kuhakiki programu (neno "programu" hujumuisha michezo) na maudhui mengine ya kidijitali. Maneno haya hushughulikia matumizi ya Duka la Office, Duka la Windows na Duka la Xbox. "Duka la Office" humaanisha Duka la bidhaa na programu za Office, Office 365, SharePoint, Exchange, Access na Project (matoleo ya 2013 au baadaye), au uzoefu mwingine wowote ambao una chapa ya Duka la Office. "Duka la Windows" humaanisha Duka la vifaa vya Windows kama vile simu, kompyuta na kompyuta kibao, au uzoefu mwingine wowote ambao una chapa ya Duka la Windows. "Duka la Xbox" humaanisha Duka la Xbox One na viweko vya Xbox 360, au uzoefu mwingine wowote ambao una chapa ya Duka la Xbox.
  • i. Masharti ya Leseni. Tutamtambua mchapishaji wa kila programu inayopatikana katika Duka husika. Isipokuwa masharti tofauti ya leseni yawe yametolea na programu, Masharti ya Kawaida ya Leseni ya Programu (""SALT"") mwisho wa Masharti haya ni makubaliano kati yako na mchapishaji wa programu yanayoweka masharti ya leseni ambayo hutumika kwa programu unayopakua kupitia Windows Store au Xbox Store. Ili kufafanua, Masharti haya yanashughulikia matumizi, na huduma zinazotolewa na Microsoft. Sehemu ya 5 ya Masharti haya hutumika pia kwa Programu na Huduma zozote za Wahusika wengine zilizopatikana kupitia Store. Programu zinazopakuliwa kupitia Duka la Office hazisimamiwi na SALT na zina masharti tofauti ya leseni ambayo yanatumika.
  • ii. Visasisho. Microsoft itakagua kiotomatiki kama kuna visasisho na kuvipakua kwenye programu zako, hata kama hujaingia kwenye Duka husika. Unaweza kubadilisha mipangilio ya Duka au mfumo wako ikiwa unapendelea kutopekea visasisho otomatiki vya programu za Duka. Hata hivyo, programu nyingine za Duka la Office ambazo zinapangishwa mtandaoni kikamilifu au nusu zinaweza kusasishwa wakati wowote na msanidi programu na huenda zisihitaji kibali chako cha kusasisha.
  • iii. Ukadiriaji na Hakiki. Ukikadiria au kuhakiki programu au Bidhaa nyingine ya Dijitali kwenye Duka, unaweza kupokea barua pepe kutoka kwa Microsoft yenye maudhui kutoka kwa mchapishaji wa programu au Bidhaa ya Dijitali. Barua pepe yoyote kama hiyo hutoka kwa Microsoft; hatushiriki anwani yako ya barua pepe na wachapishaji wengine wa programu au Bidhaa nyingine za Dijitali ulizopata kupitia Duka.
  • iv. Onyo la Usalama. Ili kuepuka jeraha lolote au macho kuchoka, unastahili kupumzika mara kwa mara baada ya kutumia programu au programu nyingine, hasa ikiwa unahisi maumivu au uchovu wowote unaotokana na matumizi. Ikiwa utahisi uchovu, unastahili kupumzika. Uchovu unaweza kujumuisha kuhisi kichefuchefu, kuhisi vibaya, kizunguzungu, kuchanganyikiwa, maumivu ya kichwa, uchovu, macho kuchoka, au macho kukauka. Kutumia programu kunaweza kukutatiza na kutatiza wengine karibu na wewe. Epuka hatari ya kuteleza, ngazi, paa zilizo chini, vifaa vinavyoweza kuvunjika upesi au vya dhamani ambavyo vinaweza kuharibiwa. Asilimia ndogo sana ya watu wanaweza kupata kifafa wanapoona picha nyingine kama taa zinazomweka au ruwaza ambazo zinaweza kuonekana kwenye programu. Hata watu wasiokuwa na historia ya kifafa huenda wakawa na hali isiyotambuliwa ambayo inaweza kusababisha kifafa. Huenda dalili zikajumuisha kizunguzungu, kutoona vizuri, mtetemo wa uso, mkutuo au mtetemko wa viungo, kukanganywa, kuchanganyikiwa, upotezaji wa fahamu, au mitukutiko. Mara moja acha kutumia na ushauriane na daktari ikiwa utahisi yoyote kati ya dalili hizi, au shauriana na daktari kabla ya kutumia programu ikiwa umewahi kupta dalali zinazohusishwa na kifafa. Wazazi wanastahili kufuatilia jinsi watoto wao wanavyotumia programu ili kuona kama kula dalili.
Maandishi kamili
Vipengele vya Familia ya MicrosoftVipengele vya Familia ya Microsoft14c_MicrosoftFamily
Muhtasari
 • c. Vipengele vya Familia ya Microsoft. Wazazi na watoto wanaweza kutumia vipengele vya Familia ya Microsoft kujenga imani kulingana na ufahamu wa kushiriki ni tabia, tovuti, programu, michezo, maeneo halisi, na matumizi gani ambao ni sahihi katika familia yao. Wazazi wanaweza kuunda Familia kwa kwenda kwenye https://account.microsoft.com/family (au kwa kufuata maagizo kwenye kifaa chao cha Windows au kiweko cha Xbox) na kuwaalika watoto au wazazi wengine kujiunga. Kuna vipengele vingi vinavyopatikana kwa wanafamilia, kwa hivyo kwa makini pitia maelezo yaliyotolewa unapokubali kuunda au kujiunga na familia na wakati unanunua Bidhaa za Dijitali kwa ajili ya ufikiaji wa familia. Kwa kuunda au kujiunga na Familia, unakubali utatumia familia kulingana na lengo lake na hutaitumia kwa njia isiyoidhinishwa ili kufikia maelezo ya mtu mwingine kinyume cha sheria.
Maandishi kamili
Ujumbe wa KikundiUjumbe wa Kikundi14d_GroupMessaging
Muhtasari
 • d. Ujumbe wa Kikundi. Huduma mbalimbali za Microsoft hukuwezesha kutuma ujumbe kwa wengine kupitia ujumbe wa sauti au SMS ("ujumbe"), na/au huruhusu Microsoft na mashirika tanzu yanayodhibitiwa na Microsoft kutuma ujumbe kama huo kwako na watumiaji wengine zaidi kwa niaba yako. UNAPOIAGIZA MICROSOFT NA MASHIRIKA TANZU YANAYODHIBITIWA NA MICROSOFT KUTUMA UJUMBE KAMA HUO KWAKO AU KWA WENGINE, UNAWAKILISHA NA KUTUHAKIKISHIA KWAMBA WEWE NA KILA MTU ULIYETUAGIZA TUMTUMIE UJUMBE ANAKUBALI KUPOKEA UJUMBE KAMA HUO NA UJUMBE MWINGINE WOWOTE UNAOHUSIANA NA USIMAMIZI KUTOKA MICROSOFT NA MASHIRIKA TANZU YANAYODHIBITIWA NA MICROSOFT. "Ujumbe unaotoka kwa wasimamizi" na ujumbe wa mara kwa mara wa shughuli kutoka kwa huduma fulani ya Microsoft, ikiwa ni pamoja na lakini sio tu "ujumbe wa kukaribishwa" au maagizo kuhusu jinsi ya kukomesha kupokea ujumbe. Ikiwa wewe au wanachama wa kikundi hamtaki kupokea ujumbe kama huo tena mnaweza kuchagua kutopokea ujumbe zaidi kutoka Microsoft au mashirika tanzu yanayodhibitiwa na Microsoft wakati wowote ule kwa kufuata maagizo yaliyotolewa hapa. Ikiwa hutaki tena kupokea ujumbe kama huo au kushiriki katika kikundi, unakubali kwamba utachagua kujiondoa kwenye wanaopokea kupitia maagizo yaliyotolewa na programu au huduma husika. Ikiwa una sababu ya kuamini kwamba mwanachama wa kikundi hataki kupokea ujumbe kama huo tena au kuhusika katika kikundi, unakubali kumwondoa kwenye kikundi. Unawakilisha na kutuhakikishia pia kwamba wewe na kila mtu uliyetuagiza tumtumie ujumbe anafahamu kwamba kila mwanachama wa kikundi anawajibika kwa gharama za ujumbe wowote uliotathminiwa na mtoa huduma wake wa simu ya mkononi, ikiwa ni pamoja na gharama zozote za kimataifa za ujumbe ambazo zinaweza kutumika wakati ujumbe unapitishwa kutoka kwa nambari za Marekani.
Maandishi kamili
Skype na GroupMeSkype na GroupMe14e_Skype
Muhtasari
 • e. Skype na GroupMe.
  • i. Hakuna Ufikiaji wa Huduma za Dharura. Kuna tofauti muhimu kati ya huduma za zamani za simu na Skype. Skype haihitajiki kutoa ufikiaji wa Huduma za Dharura chini ya sheria yoyote husika ya nchini au kanuni, masharti au sheria za kitaifa. Programu na bidhaa za Skype hazikusudiwi kuunga mkono au kubeba simu za dharura za hospitali za aina zozote, mawakala wa utekelezaji wa sheria, vitengo vya huduma za matibabu au huduma nyingine ya aina yoyote ambayo huunganisha mtumiaji kwa mfanyakazi wa huduma za dharura au maeneo ya kujibu ya usalama wa umma ("Huduma za Dharura"). Unakiri na kukubali kwamba: (i) Ni jukumu lako kununua huduma za kawaida za simu pasiwaya (ya mkononi) au simu yenye waya ambayo hutoa ufikiaji wa Huduma za Dharura; na (ii) Skype haibadilishi huduma yako msingi ya simu.
  • ii. API au Utangazaji. Ikiwa unataka kutumia Skype kuhusiana na utangazaji wowote, lazima uafikiane na "TOS ya Utangazaji" iliyo https://www.skype.com/go/legal.broadcast. Ikiwa unataka kutumia kiolesura chochote cha programu ("API") kiliopo au kinachopatikana kupitia Skype lazima ufuate masharti husika ya leseni, ambayo yanaptikana kwenye www.skype.com/go/legal.
  • iii. Sera za Matumizi ya Haki. Huenda sera za matumizi ya haki zikatumika kwa matumizi yako ya Skype. Tafadhali hakiki sera hizi ambazo zimebuniwa kulinda dhidi ya ulaghai na matumizi mabaya na yanaweza kuweka vikomo kwa aina, muda, au viwango vya simu au ujumbe unaoweza kutuma. Sera hizi zimejumuishwa katika Masharti haya kwa kurejelea. Unaweza kupata sera hizi kwenye https://www.skype.com/go/terms.fairusage/.
  • iv. Ramani. Skype ina vipengele ambavyo vinakuwezesha kuwasilisha maelezo, au kujiweka kwenye ramani kwa kutumia, huduma ya ramani. Kwa kutumia vipengele hivyo, unakubaliana na Masharti haya na masharti ya Ramani za Google yanayopatikana kwenye https://www.google.com/intl/en_ALL/help/terms_maps.html au masharti kama hayo ya Google yanayopatikana katika nchi yako.
  • v. Watumiaji wa Serikali. Ikiwa unataka kutumia akaunti ya biashara na/au Meneja wa Skype kwa niaba ya Serikali ya Marekani au wakala wa Serikali ya Marekani, Masharti haya hayatumiki kwa matumizi hayo. Kwa masharti husika au maelezo ya ziada, tafadhali wasiliana na usgovusers@skype.net.
  • vi. Matumizi ya Kibinafsi/Yasio ya Kibiashara. Matumizi ya Skype ni kwa matumizi ya kibinafsi na yasiyo ya kibiashara. Unaruhusiwa kutumia Skype ukiwa kazini kwa mawasiliano yako mwenyewe ya kibiashara.
  • vii. Nambari ya Skype/Skype To Go. Ikiwa Skype inakupa Nambari ya Skype au nambari ya Skype To Go, unakubali kwamba humiliki nambari hiyo au huna haki ya kubakia na nambari hiyo milele. Katika nchi nyingine, huenda nambari ikapatikana kwako kutoka kwa mshirika wa Skype badala ya Skype, na huenda ukahitaji kuingia kwenye makubaliano tofauti na mshirika kama huyo.
  • viii. Msimamizi wa Skype. "Akaunti ya Msimamizi wa Skype" hufunguliwa na kusimamiwa na wewe, ukiwa kama msimamizi wa kikundi cha Skype Manager na wala sio shirika la biashara. Unaweza kuunganisha akaunti yako binafsi ya Microsoft kwenye kikundi cha Skype Manager ("Akaunti Iliyounganishwa"). Unaweza kuwateua wasimamizi wa ziada kwenye kikundi chako cha Skype Manager ikiwa watakubali Masharti haya. Ukiteua Nambari za Skype kwenye Akaunti Iliyounganishwa, unawajibika kuafikiana na mahitaji yoyote yanayohusiana na makazi au eneo la watumiaji wa Akaunti zako Zilizounganishwa. Ukichagua kutounganisha Akaunti Iliyounganishwa kwenye kikundi cha Skype Manager, usajili wowote ulioteuliwa au Karadha za Skype au Nambari za Skype hazitaweza kupatikana na Maudhui Yako au nyenzo zinazohusishwa na akaunti isiyounganishwa hazitaweza kupatikana tena. Unakubali kuchakata maelezo yoyote ya kibinafsi ya watumiaji wako wa Akaunti Iliyounganishwa kulingana na sheria zote husika za kulinda data.
  • ix. Gharama za Skype. Bei zote za bidhaa zilizolipwa za Skype zinajumuisha ushuru husika, isipokuwa iwe imesemekana kivingine. Gharama inayolipishwa ya kupiga simu nje ya usajili huwa na ada ya muunganisho (hulipishwa mara moja kwa kila simu) na kiasi cha kila dakika kama iliyowekwa kwenye www.skype.com/go/allrates. Gharama za simu zitapunguzwa kwenye salio lako la Karadha ya Skype. Huenda Skype ikabadilisha kiwango chake cha ada ya kupiga simu wakati wowote kwa kuchapisha mabadiliko kama hayo kwenye www.skype.com/go/allrates. Viwango vipya vitatumika kwa simu yako ifuatayo baada ya machapisho ya viwango vipya. Tafadhali angalia viwango vipya kabla ya kupiga simu yako. Dakika za simu za vipeo sehemu na gharama za vipeo sehemu zitajumlishwa na kuwa kizio kamili. Katika baadhi ya nchi, bidhaa zilizolipwa za Skype hutolewa na mshirka wa Skype wa eneo hilo na masharti ya matumizi ya mshirika huyo yatatumika kwa shughuli kama hizo.
  • x. Karadha za Skype. Skype haihakikishi kwamba utaweza kutumia salio lako la Karadha za Skype ili kununua bidhaa zote zinazolipiwa za Skype. Ukikosa kutumia Karadha zako za Skype kwa kipindi cha siku 180, Skype itaweka Karadha zako za Skype kwa hali ya isiyotumika. Unaweza kuamilisha upya Karadha za Skype kwa kufuata kiungo cha uamilishaji upya kwenye https://www.skype.com/go/store.reactivate.credit. Ikiwa uko nchini Japani na ununue Karadha zako za Skype kutoka kwa tovuti ya Skype, sentensi mbili zinazofuata hazitumiki kwako na Karadha yako ya Skype itaisha muda wake katika siku 180 baada ya tarehe ya ununuzi. Mara tu karadha yako inapoisha muda wake, hutaweza tena kuiamilisha upya au kuitumia. Unaweza kuwezesha kipengele cha Kuongeza karadha Kiotomatiki wakati unaponunua Karadha za Skype kwa kuweka tiki kisanduku kinachofaa. Ikiwezeshwa, salio lako la Karadha za Skype litaongezwa upya na kiasi sawa na mbinu yako uliyochagua ya malipo kila wakati salio lako la Skype linapokuwa chini ya kigezo kilichowekwa na Skype mara kwa mara. Ikiwa ulinunua usajili na mbinu ya malipo kando na kadi ya mkopo, PayPal au Moneybookers (Skrill), na umewezesha Kuongeza karadha Kiotomatiki, salio lako la Karadha za Skype litaongezwa upya na kiasi kinachofaa ili kununua usajili wako ufuatao unaoendelea. Unaweza kulemaza Kuongeza karadha Kiotomatiki wakati wowote kwa kufikia na kubadilisha mipangilio yako katika kituo cha akaunti yako katika Skype.
  • xi. Ada ya Ujumbe wa Kimataifa. Kwa sasa GroupMe inatumia nambari za Marekani kwa kila kikundi kinachobuniwa. Kila ujumbe wa maandishi unaotumwa au kupokewa kutoka kwa nambari ya GroupMe utachukuliwa kama ujumbe wa maandishi wa kimataifa uliotumwa au kupokewa kutoka Marekani. Tafadhali wasiliana na mtoa huduma wako kwa ada husika za kimataifa.
  • xii. Tuma na upokee pesa. Kwa kutumia kipengele cha kutuma na kupokea pesa (ikiwa kinatumika), unakubali kwamba Skype hutumia wahusika wengine kutoa huduma za malipo na kutekeleza uhawilisho. Skype haitoi huduma za malipo au kutekeleza uhawilisho na haiko katika biashara ya huduma za pesa. Kutuma na kupokea pesa kwenye Skype kunaweza kupatikana tu kwa watumiaji ambao wana umri wa miaka 18 na zaidi (au kulingana na masharti ya wahusika wengine) na wanaojisajili na wameidhinishwa kupata akaunti na mtoa huduma mwingine. Ili kutumia kipengele cha kutuma pesa, huenda ukahitajika kukubali sheria na masharti ya wahusika wengine na kutoa vibali vya kushiriki data na washirika wengine kwa malengo ya kutoa huduma. Kama Skype itapokea ilani kwamba matumizi yako ya kipengele cha kutuma pesa yanakiuka sheria na masharti ya wahusika wengine, huenda Skype ikachukua hatua dhidi ya akaunti yako, kama vile kukatisha au kusitisha akaunti yako. Skype, au Microsoft, haitawajibika kwa huduma za malipo zinazotolewa na wahusika wengine au hatua zozote zilizochukuliwa chini ya sheria na masharti ya wahusika wengine. Skype haitoi udhamini, uwakilishi au uhakikisho kwamba kipengele cha kutuma na kupokea pesa kitapatikana au kuendelea kupatikana.
Maandishi kamili
Bing na MSNBing na MSN14f_BingandMSN
Muhtasari
 • f. Bing na MSN.
  • i. Nyenzo za Bing na MSN. Makala, maandishi, picha, ramani, video, vichezaji video na nyenzo za wahusika wengine zinazopatikana kwenye Bing na MSN, ikiwa ni pamoja na kupitia boti, programu na mipango ya Microsoft, ni za matumizi yako binafsi tu na wala sio ya kibiashara. Matumizi mengine, ikiwa ni pamoja na upakuaji, kunakili au usambazaji wa nyenzo hizi, au kutumia nyenzo au bidhaa hizi kuunda bidhaa zako mwenyewe, zimeruhusiwa tu kwa umbali uliobainishwa na Microsoft au wamiliki walioidhinishwa, au kuruhusiwa na sheria husika ya hakimiliki. Microsoft au wamiliki wengine wa haki wana haki zote za nyenzo zisizotolewa moja kwa moja na Microsoft chini ya masharti ya leseni, iwe kwa kuhusika, katazo, au kivingine.
  • ii. Ramani za Bing. Huenda usiweze kutumia picha ya mwonekano wa Juu wa Marekani, Kanada, Meksiko, Nyuzilandi, Australia, au Japani kwa matumizi ya kiserikali bila kibali chetu kilichoandikwa kando.
  • iii. Bing Places na Bing Manufacturer Center. Unapotoa Data yako au Maudhui Yako kwa Bing Places au Bing Manufacturer Center, unaipa Microsoft leseni ya mali-akili isiyokuwa na mrahaba ya duniani kote ya kutumia, kuzalisha, kuhifadhi, kurekebisha, kukusanya, kukuza, kupitisha, kuonyesha au kusambaza kama sehemu ya huduma, na kutoa leseni nyingine ya haki hizo kwa wahusika wengine.
Maandishi kamili
CortanaCortana14g_Cortana
Muhtasari
 • g. Cortana.
  • i. Matumizi ya Kibinafsi Yasio ya Kibiashara. Cortana ni Huduma ya usaidizi wa kibinafsi kutoka Microsoft. Vipengele, huduma, maudhui na Programu na Huduma za Wahusika Wengine zinazotolewa na Cortana (kwa pamoja "Huduma za Cortana") ni za kwa matumizi yako ya kibinafsi pekee na yasiyo ya kibiashara.
  • ii. Utendaji na Maudhui. Cortana hutoa vipengele mbalimbali, baadhi ambazo zimebinafsishwa. Huduma za Cortana zinaweza kukuruhusu kufikia huduma, maelezo au utendakazi unaotolewa na Huduma nyingine za Microsoft au Programu na Huduma za Wahusika Wengine. Masharti ya huduma maalum ya sehemu ya 13 pia hutumika kwenye matumizi yako ya Huduma husika za Microsoft zinazofikiwa kupitia Huduma za Cortana. Cortana hutoa maelezo haya kwa malengo yako ya upangaji tu na unapaswa kuwa mwangalifu wewe mwenyewe wakati unahakiki na kutegemea maelezo haya. Microsoft haihakikishi usahihi, uthabiti, upatikanaji au umilele wa uzoefu uliobinafsishwa unaotolewa na Cortana. Microsoft haiwajibiki ikiwa kipengele cha kudhibiti mawasiliano ya Cortana kitachelewesha au kukuzuia dhidi ya kupokea, kuhakiki au kutuma mawasiliano au taarifa.
  • iii. Programu na Huduma za Wahusika Wengine. Kama sehemu ya kutoa Huduma za Cortana, Cortana inaweza kubadilisha maelezo na Programu na Huduma za Wahusika Wengine, kama vile msimbo wako wa zip na maswali na majibu yaliyorejeshwa na Programu na Huduma za Wahusika Wengine, ili kutimiza ombi lako. Kupitia kuunganisha akaunti, Cortana inaweza kuwawezesha watumiaji kununua kupitia Programu na Huduma za Wahusika Wengine kwa kutumia mapendeleo na mipangilio ya akaunti ambayo mtumiaji ameweka moja kwa moja na Programu na Huduma hizo za Wahusika Wengine. Watumiaji wanaweza kutenganisha kuunganishwa kwa akaunti wakati wowote. Matumizi yako ya Programu na Huduma za Wahusika wengine yamesimamiwa chini ya sehemu ya 5 ya Masharti haya. Wachapishaji wa Programu na Huduma za Wahusika Wengine wanaweza kubadilika au kukatisha utendakazi au vipengele vya Programu na Huduma zao za Wahusika Wengine au ujumuishaji wa Huduma za Cortana. Microsoft haiwajibiki kwa programu au programu ndogo inayotolewa na mtengenezaji.
  • iv. Vifaa Vilivyowezeshwa Cortana. Vifaa vilivyowezeshwa Cortana ni bidhaa au vifaa ambavyo vimewezeshwa kufikia Huduma za Cortana, au bidhaa au vifaa ambavyo vinatangamana na Huduma za Cortana. Vifaa vilivyowezeshwa Cortana ni pamoja na vifaa au bidhaa za wahusika wengine ambazo Microsoft inamiliki, kutengeneza, au kuunda. Microsoft haiwajibiki kwa vifaa au bidhaa hizi za wahusika wengine.
  • v. Visasisho vya Programu. Kwa kifaa chochote ambacho kinaweza kuunganishwa kwenye Huduma za Cortana, tunaweza kukagua kiotomatiki toleo lako la programu ya Huduma za Cortana na kupakua visasisho vya programu au mabadiliko ya usanidi au kuhitaji watengenezaji wowote wa vifaa vilivyowezeshwa Cortana kuweka huduma za Cortana zikiwa zimesasishwa.
Maandishi kamili
Outlook.comOutlook.com14h_Outlook_com
Muhtasari
 • h. Outlook.com. Anwani ya barua pepe ya Outlook.com (au @msn, @hotmail, au @live) ambayo unatumia kufundua akaunti yako ya Microsoft itakuwa ya kipekee kwako bora kisanduku pokezi cha Outlookcom au akaunti ya Microsoft bado inatumika. Katika tukio kwamba kisanduku chako pokezi cha Outlook.com au akaunti ya Microsoft imefungwa na wewe au na Microsoft kulingana na Masharti haya, anwani ya barua pepe au jina la mtumiaji linaweza kutumiwa tena katika mfumo wetu na kupangiswa mtumiaji mwingine.
Maandishi kamili
Huduma za OfficeHuduma za Office14i_officeBasedServices
Muhtasari
 • i. Huduma za Office. Office 365 Home, Office 365 Personal, Office 365 University, Office Online, Sway, OneNote.com na usajili mwingine wowote wa Office 365 au Huduma zenye chapa ya Office ni za matumizi ya kibinafsi, yasio ya kibiashara, isipokuwa uwe una haki za kibiashara chini ya makubaliano mengine na Microsoft.
Maandishi kamili
Huduma za Microsoft HealthHuduma za Microsoft Health14j_MicrosoftHealthServices
Muhtasari
 • j. Huduma za Microsoft Health.
  • i. HealthVault. HealthVault imekusudiwa uhifadhi maelezo yako ya kibinafsi yanayohusiana na afya na maelezo kuhusu watu wengine (kama vile familia ykao) kwa kibali chao. Akaunti za HealthVault hazistahili kutumiwa na watoa huduma za afya au kwa malengo mengine ya kibiashara au yasio ya kibinafsi. Maelezo katika akaunti yako huenda yasiwe sahihi au yamesasishwa na yanastahili kuangalia na mtoa huduma yeyote wa afya kama maelezo tu. Huduma ya HealthVault haina rekodi zozote za watoa huduma ya afya au malengo mengine ya matibabu au usimamiaji kesi. Kwa mfano, rekodi za HeathVault sio seti za rekodi zilizoteuliwa kama ilivyofafanuliwa chini ya masharti ya Marekani. Ikiwa mtoa huduma ya afya ataamua kujumuisha data yoyote inayopatikana kwenye HeathVault katika rekodi zake, anastahili kuhifadhi nakala katika mfumo wake mwenyewe. Ikiwa kuna mtunzaji mwenza wa rekodi katika akaunti yako (kwa sababu mmoja wenyu alimwalika mwingine), unakubali kwamba mtunzaji huyo mwenza ana udhibiti kamili wa rekodi hiyo na anaweza kukatisha ufikiaji wako wa rekodi, kudhibiti ufikiaji wa watu wengine wa rekodi hiyo, na kutazama data ya rekodi ikiwa ni pamoja na ni lini rekodi ilitumika. Microsoft haikubali sifa zisizo za Microsoft (kama vile Facebook na OpenID), kwa hivyo usaidizi wa wateja wa HeathVault hautaweza kusaidia na matatizo kama hayo ya kuingia. Ukipoteza sifa zako za kuingia, au ikiwa akaunti uliyopata sifa zako itafunga, hutaweza kurejesha data yako iliyohifadhiwa. Ili kusaidia kudumisha ufikiaji, tunapendekeza utumie zaidi ya sifa moja ya kuingia kwa akaunti yako ya HealthVault. Microsoft haiidhinishi au kudhibiti, na haiwajibiki kwa shughuli, usaidizi, au usalama wa sifa zisizo za Microsoft ambazo unaweza kutumia.
  • ii. Microsoft Band. Kifaa na programu ya Microsoft Band sio vifaa vya matibabu na vinakusudiwa kwa malengo ya mazoezi na ubora tu. Havijaundwa au kukusudiwa kutumika kutambua magonjwa au hali nyingine, au kutibu, kupunguza makali, matibabu, au kuzuia magonjwa au hali nyingine. Microsoft haiwajibiki kwa uamuzi wowote unaofanya kulingana na maelezo unayopokea kutoka Microsoft Band.
Maandishi kamili
Bidhaa za KidijitaliBidhaa za Kidijitali14k_DigitalGoods
Muhtasari
 • k. Bidhaa za Dijitali. Kupitia Microsoft Groove, Filamu na TV ya Microsoft, Duka na huduma nyingine husika na za baadaye, Microsoft itakuwezesha kupata, kusikiliza, kuona, kucheza au kusoma (kulingana na hali) muziki, picha, video, maandishi, vitabu, michezo au nyenzo nyingine ("Bidhaa za Kidijitali") ambazo unaweza kupata katika hali ya kidijitali. Bidhaa za Kidijitali ni za matumizi yako ya kibinafsi na burudani isiyo ya kibiashara tu. Unakubali kutosambaza, kutangaza, kufanya au kuonyesha hadharani au kuhamisha nakala zozote za Bidhaa za Dijitali. Bidhaa za Dijitali zinaweza kuwa zinamilikiwa na Microsoft au wahusika wengine. Hata hivyo, katika hali zote, unafahamu na kukubali kwamba haki zako kuhusiana na Bidhaa za Kidijitali zimezuiwa na Masharti haya, sheria ya hakimiliki, na kanuni za matumizi yaliyo katika https://go.microsoft.com/fwlink/p/?LinkId=723143. Unakubali kwamba hutajaribu kurekebisha Bidhaa zozote za Kidijitali zilizopatikana kupitia Huduma zozote kwa madhumuni yoyote yale, ikiwa ni pamoja na lengo la kuficha au kubadilisha umiliki au chanzo cha Bidhaa hizo za Kidijitali. Mara kwa mara, Microsoft au wamiliki wa Bidhaa za Kidijitali wanaweza kuondoa Bidhaa za Kidijitali kutoka kwenye Huduma bila ilani.
Maandishi kamili
OneDriveOneDrive14l_OneDrive
Muhtasari
 • l. OneDrive.
  • i. Mgao wa Hifadhi. Ikiwa una maudhui mengi yaliyohifadhiwa kwenye akaunti yako ya OneDrive zaidi ya ulivyopewa chini ya masharti ya huduma yako ya usajili isiyolipishwa au inayolipishwa ya OneDrive na usijibu ilani kutoka kwa Microsoft ya kutatua akaunti yako kwa kuondoa maudhui yaliyozidi au kuhamia mpango mpya wa usajili wenye hifadhi zaidi, tuna haki ya kufunga akaunti yako na kufuta au kulemaza idhini yako ya kufikia Maudhui Yako kwenye OneDrive.
  • ii. Utendakazi wa Huduma. Wakati mwingine utapata ucheleweshaji katika kupakia au kulandanisha maudhui kwenye OneDrive kwa kutegemea mambo kama vile vifaa vyako, muunganisho wa intaneti na juhudi za Microsoft za kudumisha utendakazi na uadilifu wa huduma zake.
Maandishi kamili
Microsoft RewardsMicrosoft Rewards14m_MicrosoftRewards
Muhtasari
 • m. Microsoft Rewards.
  • i. Mpango. Microsoft Rewards ("Mpango") hukuwezesha kupata pointi unazoweza kukomboa kwa shughuli, kama vile utafiti, ununuzi unaofaa, muda uliochukuliwa kuvinjari na Microsoft Edge, na matoleo mengine kutoka Microsoft. Matoleo yanayoweza kutofautiana kulingana na soko. Utafutaji ni tendo la mtumiaji kuingiza matini yeye mwenyewe kwa nia njema ya kupata matokeo ya utafutaji ya Bing kwa malengo binafsi ya mtumiaji ya utafutaji na haijumuishi swali lolote lililoingizwa na boti, makro, au njia nyingine otomati au za ulaghai za aina yoyote ("Utafutaji"). Ununuzi ni mchakato wa kununua bidhaa au upakuaji na kupata leseni ya maudhui ya dijitali kutoka Microsoft, iwe hayana malipo au yanayolipiwa ("Ununuzi"). Alama za Rewards hazitolewi kwa kila ununuzi kutoka Microsoft. Kuvinjari na Microsoft Edge humaanisha kuwa na kivinjari kwenye skrini ya kifaa chako (k.m. kimefunguliwa na kinatumika hadi ikoni ya Microsoft Edge imeangaziwa kwenye mwambaa wa kazi, inayoashiria kwamba programu inatumika kwa sasa), na kutumia kivinjari kutazama tovuti, kutazama video katika kivinjari, kuangalia barua pepe, au matumizi mengine ambayo vivinjari vinatumika. Ili kupata pointi kwa kutumia Microsoft Edge, lazima Bing iwekwe kama injini chaguo-msingi ya utafutaji ya kivinjari na lazima telemetri iwezeshwe katika mipangilio yako ya Windows. Huenda Microsoft ikakupa nafasi zaidi za kupata pointi mara kwa mara, na kila toleo la kupata pointi halitapatikana milele. Pointi zako ulizopata zinaweza kukombolewa kwa vipengee ("Rewards") katika ukurasa wa kukomboa. Kwa maelezo zaidi angalia sehemu ya Rewards kwenye support.microsoft.com ("Maswali Yanayoulizwa Sana").
   • 1. Mahitaji ya Mpango. Unahitaji akaunti halali ya Microsoft na lazima vifaa vyako vifikie mahitaji msingi ya mfumo. Mpango huu umefunguliwa kwa watumiaji wanaoishi masoko yaliyoorodheshwa katika Maswali Yanayoulizwa Sana. Mtu hawezi kuwa na zaidi ya akaunti moja ya Mpango, hata kama mtu huyo ana anwani kadhaa za barua pepe, na kaya imezuiwa kwa akaunti sita. Mpango huu ni wa matumizi ya kibinafsi na yasiyo ya kibiashara pekee.
   • 2. Pointi. Isipokuwa kwa kuchangia pointi zako kwa shiriki lisilokuwa la faida lililoorodheshwa kwenye kituo cha ukomboaji, huwezi kuhamisha pointi. Pointi si rasilimali yako binafsi, na huenda usiweze kupata pesa zozote kwa kuzibadilisha. Unapata pointi kwa msingi wa matangazo. Huwezi kununua pointi. Huenda Microsoft ikazuia wingi wa pointi au Rewards kwa kila mtu, kwa kila kaya, au kwa muda uliowekwa (k.m., siku). Huwezi kukomboa zaidi ya pointi 550,000 kwa kila mwaka wa kalenda katika Mpango. Pointi ulizopata katika Mpango si halali, na haziwezi kutumika katika mchanganyiko na, programu nyingine yoyote inayotolewa na Microsoft au wahusika wengine. Pointi ambazo haziwezi kukombolewa huisha muda wake ukikosa kupata au kukomboa pointi zozote kwa miezi 18.
   • 3. Rewards. Unaweza kukomboa pointi zako kwa kutembelea kituo cha ukomboaji au unaweza kuchangia pointi kwa shirika lililoorodheshwa lisilokuwa la faida. Huenda kukawa na idadi ndogo inayopatikana ya Reward maalum, na Rewards hizo zitawasilishwa kwa msingi wa anayekuja kwanza ndiye atakaye hudumiwa. Huenda ukahitajika kutoa maelezo ya ziada, kama vile anwani yako ya barua pepe na nambari ya simu (kando na VOIP au nambari isiyolipishwa), na huenda pia ukaulizwa kuingiza msimbo wa kuzuia ulaghai au kutia saini nyaraka za ziada za kisheria ili kukomboa pointi za Rewards. Ukiagiza Reward, huwezi kuikatisha au kuirejesha ili kupata fidia ya pointi isipokuwa wakati kuna bidhaa zenye kasoro au kama inavyohitajika na sheria husika. Ukiagiza Reward ambayo imeisha au haipatikani kwa sababu nyingine iliyobainishwa na Microsoft katika uamuzi wake, tunaweza kubadilisha Reward ya thamani inayoweza kulinganishwa au kurejesha pointi zako. Microsoft inaweza kusasisha Rewards zinazotolewa katika kituo cha ukomboaji au kukomesha kutoa Rewards maalum. Huenda baadhi ya Rewards zikawa na mahitaji ya kustahiki. Mahitaji yoyote kama hayo yatajumuishwa katika toleo husika. Unawajibika kwa ushuru wote wa serikali, jimbo na wa ndani na gharama zozote zingine za kukubali na kutumia Reward. Rewards zitatumwa kwako kwenye anwani ya barua pepe uliyotoa wakati wa kuagiza Reward yako, kwa hivyo sasisha barua pepe yako. Rewards ambazo hazijawasilishwa hazitatolewa tena na kwa hivyo zitapotea. Rewards si za kuuzwa tena.
   • 4. Kughairi Kushiriki Kwako katika Mpango. Akaunti yako ya Mpango itakatishwa ukikosa kuingia angalau mara moja katika kipindi cha miezi 18. Kuongezea, Microsoft inahifadhi haki ya kukatisha akaunti ya Mpango ya mtumiaji maalum kwa kutatiza, kutumia vibaya au kulaghai Mpango huu, au kwa kukiuka Masharti haya. Baada ya Mpango kukatishwa (na wewe au sisi) au kama Mpango utakatishwa, utahitaji siku 90 kukomboa pointi zako; la sivyo, pointi hizo zitapotea. Wakati wa ukatishaji, haki yako ya kutumia Mpango na pointi zilizolimbikizana za baadaye zitaisha.
   • 5. Hali Nyingine. Microsoft inahifadhi haki ya kukuzuia; kulemaza ufikiaji wako wa Mpango au akaunti yako ya Rewards; na/au kushikilia pointi, Rewards na michango ya ufadhili, ikiwa Microsoft inaamini unaingilia au kutumia vibaya hali yoyote ya Mpango au unaweza kuwa unashiriki katika shughuli ambazo zinakiuka Masharti haya.
Maandishi kamili
MchanganyikoMchanganyiko16_17_18_miscellaneous
Muhtasari

14. Mchanganyiko. Sehemu hii, na sehemu za 1, 9 (kwa viwango vilivyopatikana kabla ya mwisho wa Masharti haya), 10, 11, 12, 15, 17 na zile kwa masharti yake zinatumika baada ya Masharti haya kuisha zitaponea usitishaji au ukatishaji wa makubaliano haya. Kwa kiasi kinachoruhusiwa na sheria husika, huenda tukatumia Masharti haya, tukatoa mkataba mwingine wa majukumu yetu chini ya Masharti haya, au kutoa leseni nyingine ya masharti yetu chini ya Masharti haya, ikiwa yote au sehemu yake, wakati wowote bila kukupa ilani. Huwezi kupangia Masharti haya au kuhamisha haki zozote za kutumia Huduma. Haya ndiyo makubaliano yote kati yako na Microsoft kwa matumizi yako ya Huduma. Yamechukua nafasi ya makubaliano yote ya mapema kati yako na Microsoft kuhusiana na matumizi yako ya Huduma. Kwa kukubaliana na Masharti haya, hujategemea taarifa, uwakilishaji, waranti, ufahamu, shughuli, ahadi au thibitisho lolote kando na lililowekwa hapa moja kwa moja katika Masharti haya. Sehemu zote za Masharti haya yanatumika kwa upeo unaoruhusiwa na sheria husika. Ikiwa mahakama au msuluhishi itasema kwamba hatuwezi kutekeleza sehemu ya Masharti haya kama ilivyoandikwa, tunaweza kubadilisha maneno hayo na maneno mengine kama hayo kwa kiwango kinachoweza kutekelezwa chini ya sheria husika, lakini salio lingine la Masharti halitabadilika. Masharti haya ni ya kukunufaisha wewe na sisi tu. Masharti haya si ya kumfaidi mtu mwingine, isipokuwa warithi na wateuliwa wa Microsoft. Vichwa vya sehemu ni vya marejeo tu na havina athari ya kisheria.

15. Madai Lazima Yawasilishwe Ndani ya Mwaka Mmoja. Madai yoyote yanayohusiana na Masharti au Huduma hizi lazima yawasilishwe mahakamani (au usuluhishi ikiwa sehemu ya 10(d) inatumika) ndani ya mwaka mmoja wa tarehe ambayo ungeweza kuwasilisha madai kwa mara ya kwanza, isipokuwa sheria yako ya nchini iwe inahitaji muda zaidi wa kuwasilisha madai. Ikwia hayajawasilishwa ndani ya muda huo, basi huzuiliwa kabisa.

16. Sheria za Biasharanje. Lazima ufuate sheria na masharti yote ya nyumbani na ya kimataifa ya biasharanje ambayo yanatumika kwa programu na/au Huduma, ambazo zinajumuisha vizuizi vya mwisho, watumiaji, na matumizi. Kwa maelezo zaidi kuhusu vizuizi vya kijiografia na biasharanje, tembelea https://go.microsoft.com/fwlink/?linkid=868968 na https://www.microsoft.com/exporting.

17. Kuhifadhi Haki na Majibu. Isipokuwa kama ilivyotolewa moja kwa moja chini ya Masharti haya, Microsoft haikupatii leseni au haki nyingine za aina yoyote chini ya hataza yoyote, jinsi ya kujua, hakimiliki, siri za biashara, alama za biashara au mali yoyote ya akili inayomilikiwa au kudhibitiwa na Microsoft au chombo chochote husika, ikiwa ni pamoja na lakini haijakomea kwa jina lolote, alama ya biashara, nembo au yoyote kama hiyo. Ukipatia Microsoft wazo, pendekezo, au majibu yoyote, ikiwa ni pamoja na lakini bila kukomea kwa mawazo ya bidhaa, teknolojia, matangazo, majina ya bidhaa, majibu ya bidhaa na maboresho mapya ya bidhaa (""Majibu""), utayapatia Microsoft, bila gharama, mirabaha au majukumu mengine kwako, haki ya kutengeneza, yaliyotengenezwa, kuunda kazi ya wengine, kutumia, kushiriki na kufanya biashara na Majibu yako kwa njia yoyote na kwa lengo lolote. Hutatoa Majibu ambayo yanategemea leseni ambayo inahitaji Microsoft kutoa leseni ya programu, teknolojia au nyaraka zake kwa mhusika mwingine yeyote kwa sababu Microsoft hujumuisha Majibu yake ndani yake.

Maandishi kamili
ILANIILANINOTICES
Muhtasari

Ilani na taratibu za kudai ukiukaji wa rasilimali ya akili. Microsoft inaheshimu haki za mali ya akili za wahusika wengine. Ikiwa ungetaka kutuma ilani ya ukiukaji wa rasilimali ya akili, pamoja na madai ya ukiukaji wa hakimiliki, tafadhali tumia utaratibu wetu wa kuwasilisha Ilani ya Ukiukaji. MASWALI YOTE YASIYOLINGANA NA UTARATIBU HUU UNAOFUATA HAYATAPOKEA MAJIBU.

Microsoft hutumia michakato iliyowekwa katika Kichwa cha 17, cha Sheria ya Marekani, Sehemu ya 512 kuitikia ilani za ukiukaji wa hakimiliki. Katika hali zinazofaa, huenda Microsoft ikalemaza au kusitisha pia akaunti za watumiaji wa huduma za Microsoft ambao wanaendelea na ukiukaji.

Ilani na taratibu kuhusiana na hoja za rasilimali ya akili kuhusiana na utangazaji. Tafadhali hakiki Maelekezo yetu ya Rasilimali ya Akili kuhusiana na hoja za mali ya akili kwenye mtandao wetu wa utangazaji.

Ilani za hakimiliki na alama ya biashara, Huduma ni Hakimiliki ya © 2018 Microsoft Corporation na/au watoa huduma wake, One Microsoft Way, Redmond, WA 98052, U.S.A. Haki zote zimehifadhiwa. Microsoft na majina, nembo, na ikoni za bidhaa zote za Microsoft, programu, na huduma huenda zikawa alama za biashara au alama za biashara zilizosajiliwa za Microsoft nchini Marekani na/au nchi nyingine. Majina ya makampuni halisi na bidhaa huenda zikawa ni alama za biashara za wamiliki wake. Haki zozote ambazo hazijatolewa moja kwa moja katika Masharti haya zimehifadhiwa. Programu nyingine zinatumiwa katika seva zingine za tovuti ya Microsoft hutegemea nusu kazi ya Independent JPEG Group. Copyright © 1991-1996 Thomas G. Lane. Haki zote zimehifadhiwa. "gnuplot" programu inayotumiwa katika seva nyingine za tovuti ya Microsoft ni hakimiliki ya © 1986‑1993 Thomas Williams, Colin Kelley. Haki zote zimehifadhiwa.

Ilani ya kimatibabu. Microsoft haitoi ushauri wa kimatabu au wa huduma yoyote ile ya afya, utambuzi au matibabu. Daima tafuta ushauri wa daktari wako au mtoa huduma mwingine wa afya aliyehitimu ukiwa na maswali yoyote kuhusiana na hali ya kimatibabu, lishe, mazoezi au mpango wa afya. Kamwe usipuuze ushauri wa mtaalamu wa kimatibabu au kuchelewa kuutafuta kwa sababu ya maelezo uliyoyafikia kwenye au kupitia Huduma.

Manukuu ya hisa na data ya violezo (pamoja na thamani za violezo). © 2013 Morningstar, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Maelezo yaliyo hapa: (1) ni mali ya Morningstar na/au watoa huduma wake; (2) hayawezi kunakiliwa au kusambazwa; na (3) hayahakikishwi kuwa sahihi, kamilifu au ya muda unaofaa. Morningstar au watoa huduma wake wanawajibika kwa uharibifu au hasara zozote zinazotokana na matumizi yoyote ya maelezo haya. Utendakazi wa awali hauhakikishi matokeo ya baadaye.

Unaweza kutumia vielezo vyovyote vya Dow JonesSM, data ya violezo, au alamisho za Dow Jones kuhusiana na utoaji, uundaji, ufadhili, biashara, elimusoko, au matangazo ya vifaa vya kifedha au bidhaa za uwekezaji (kwa mfano, unyambuaji, bidhaa zilizopangwa, hazina ya uwekezaji, hazina ya ubadilishanaji fedha, uwekezaji, n.k. ambapo bei, faida na/au utendakazi wa vifaa au bidhaa ya uwekezaji inategemea, inahusiana, au imekusudiwa kufuatilia violezo vyovyote au mbadala vya violezo vyovyote) bila kutawanya makubaliano yaliyoandikwa na Dow Jones.

Ilani ya kifedha. Microsoft sio dalali/wakala au mshauri aliyesajiliwa wa uwekezaji chini ya sheria za amana za serikali ya Marekani au sheria ya amana za mamlaka mengine na haitoi ushauri kwa watu kuhusu ushauri wa uwekezaji, ununuzi, au uuzaji wa amana au bidhaa au huduma nyingine za kifedha. Hakuna chochote kilicho kwenye Huduma hizi ni toleo au ombi la kununua au kuuza amana yoyote. Microsoft au watoa leseni wake wa manukuu ya hisa au data ya violezo hawaidhinishi au kupendekeza bidhaa au huduma zozote maalum za kifedha. Hakuna chochote katika Huduma kimekusudiwa kuwa ushauri wa kitaalamu, ikiwa ni pamoja na, lakini haijakomea kwa, ushauri wa uwekezaji au ushuru.

Ilani kuhusu Kiwango cha Kuona cha H.264/AVC, MPEG-4 na Viwango vya Video za VC-1. Huenda programu ikajumuisha kiwango cha Kuona cha H.264/AVC, MPEG-4 na/au teknolojia ya kodeki ya VC-1 iliyotolewa leseni na MPEG LA, L.L.C. Teknolojia hii ni umbizo la ufinyazi wa data wa maelezo ya video. MPEG LA, L.L.C. inahitaji ilani hii:

BIDHAA HII INA LESENI CHINI YA LESENI ZA HATAZA ZA H.264/AVC, KUONEKANA KWA MGEG-4, NA VC-1 KWA MATUMIZI BINAFSI NA YASIYO YA KIBIASHARA KWA MTUMIAJI (A)KUSIMBUA VIDEO KULINGANA NA VIWANGO VYA ("VIWANGO VYA VIDEO") NA/AU (B) KIFICHUA H.264/AVC NA VIDEO YA VC-1 AMBAYO ILISIMBULIWA NA MTUMIAJI ANAYEHUSIKA KATIKA SHUGHULI BINAFSI NA ISIYO YA KIBIASHARA NA/AU ILIPATIKANA KUTOKA KWA MTOA VIDEO MWENYE LESENI YA KUTOA VIDEO KAMA HIYO. HAKUNA YOYOTE KATI YA LESENI HIZI ZINAJUMUISHA BIDHAA YOYOTE NYINGINE HAIJALISHI KAMA BIDHAA KAMA HIYO IMEJUMUISHWA NA PROGRAMU HII KATIKA MAKALA YOYOTE. HAKUNA LESENI ILIYOTOLEWA AU ITAKAYODOKEZWA KWA MATUMIZI MENGINE YOYOTE. MAELEZO YA ZIADA YANAWEZA KUPATIKANA KUTOKA KWA MPEG LA, L.L.C. ANGALIA TOVUTI YA MPEG LA.

Kwa malengo ya ufafanuzi tu, ilani hii haizuii au kukataza matumizi ya programu iliyotolewa chini ya Masharti haya kwa matumizi ya biashara ya kawaida ambayo ni ya kibinafsi kwa biashara hiyo ambayo haijumuishi (i) usambazaji upya wa programu kwa wahusika wengine, au (ii) uundaji wa nyenzo zenye teknolojia zinazoafikiana na VIWANGO VYA VIDEO kwa usambazaji kwa wahusika wengine.

Maandishi kamili
MASHARTI YA LESENI YA PROGRAMU YA KAWAIDAMASHARTI YA LESENI YA PROGRAMU YA KAWAIDASTANDARDAPPLICATIONLICENSETERMS
Muhtasari

MASHARTI YA LESENI YA PROGRAMU YA KAWAIDA

MICROSOFT STORE, WINDOWS STORE, NA XBOX STORE

Masharti haya ya leseni ni makubaliano kati yako na mchapishaji wa programu. Tafadhali yasome. Hutumika kwenye programu unazopakua kutoka Microsoft Store, Windows Store au Xbox Store (kila moja inayorejelewa katika masharti haya ya leseni kama "Store"), ikiwemo masasisho au nyongeza zozote za programu, isipokuwa programu ije na masharti tofauti, ambapo masharti hayo hutumika.

KWA KUPAKUA AU KUTUMIA PROGRAMU, AU KUJARIBU KUFANYA YOYOTE KATI YA HIZI, UNAKUBALI MASHARTI HAYA. UKIKOSA KUYAKUBALI, HUNA HAKI NA HUSTAHILI KUPAKUA AU KUTUMIA PROGRAMU.

Mchapishaji wa programu inamaanisha shirika linalokupa leseni, kama ilivyobainishwa katika Store.

Ukifuata masharti haya ya leseni, huna haki zilizo hapa chini.

 • 1. HAKI ZA USAKINISHAJI NA MATUMIZI; MUDA WA KUISHA. Unaweza kusakinisha na kutumia programu kwenye vifaa vya Windows au viweko vya Xbox kama ilivyofafanuliwa katika Kanuni zetu za Matumizi za Microsoft. Microsoft inahifadhi haki ya kurekebisha Kanuni za Matumizi za Microsoft wakati wowote.
 • 2. HUDUMA ZA INTANETI.
  • a. Kibali cha Huduma za Intaneti au Pasiwaya. Ikiwa programu huunganisha kwenye mifumo ya kompyuta kupitia Intaneti, ambazo zinaweza kujumuisha kupitia mtandao pasiwaya, kutumia programu hutumika kama kibali chako cha upitishaji wa maelezo ya kawaida ya vifaa (pamoja na lakini haijazuiliwa kwa maelezo ya kiufundi kuhusu kifaa chako, mfumo na programu, na vifaa vingine) kwa huduma za Intaneti au pasiwaya. Ikiwa masharti mengine yamewasilishwa kuhusiana na matumizi yako ya huduma zilizofikiwa kwa kutumia programu, masharti hayo yanatumika pia.
  • b. Kutumia vibaya Huduma za Intaneti. Huwezi kutumia huduma ya Intaneti kwa njia yoyote ambayo inaweza kuiharibu au kulemaza matumizi ya mtu yeyote au mtandao pasiwaya. Huwezi kutumia huduma ili kujaribu kufikia huduma, data, akaunti, au mtandao wowote kwa njia yoyote ile bila idhini.
 • 3. UTATHMINI WA LESENI. Programu ina leseni, haiuzwi. Makubaliano haya hukupa tu baadhi ya haki za kutumia programu. Ikiwa Microsoft italemaza uwezo wa kutumia programu kwenye kifaa chako kulingana na makubaliano yako na Microsoft, haki zozote husika za leseni zitasitishwa. Mchapisha programu anahifadhi haki nyingine zote. Isipokuwa sheria husika ikupe haki zaidi, licha ya kikwazo hiki, huenda ukatumia programu kama ilivyoruhishwa tu katika makubaliano haya. Kwa kufanya hivyo, lazima uafikiane na vizuizi vyote vya kiufundi katika programu ambavyo vinakuruhusu kuitumia tu kwa njia fulani tu. Hustahili:
  • a. Kujaribu kubadilisha vizuizi vyovyote vya kiufundi katika programu.
  • b. Kubadilisha uhandisi, kugeuza au kutenganisha programu, isipokuwa na kwa umbali tu ambao sherika husika inakubali, licha ya kikwazo hiki.
  • c. Kutengeneza nakala zaidi za programu kuliko ilivyobainishwa katika makubaliano haya au kuruhusiwa na sheria husika; licha ya kikwazo hiki.
  • d. Kuchapisha au kufanya programu ipatikane kwa wengine ili wanakili.
  • e. Kukodisha, kupangisha au kuazima programu.
  • f. Uhamishaji wa programu au makubaliano haya kwa mhusika mwingine yeyote.
 • 4. NYARAKA. Ikiwa nyaraka zimetolewa pamoja na programu, unaweza kunakili na kutumia nyaraka kwa malengo yako ya kibinafsi, na ya kurejelea.
 • 5. TEKNOLOJIA NA VIZUIZI VYA BIASHARANJE. Heunda programu ikategemea udhibiti wa teknolojia wa Marekani au wa kimataifa au sheria na masharti ya biasharanje. Lazima uafikiane na sheria na masharti yote ya kinyumbani na ya kimataifa ya biasharanje ambayo hutumika kwa teknolojia inayotumiwa au kukubaliwa na programu. Sheria hizi zinajumuisha vizuizi vya nchi, watumiaji, na matumizi. Kwa maelezo kuhusu bidhaa zenye chapa ya Microsoft, nenda kwa tovuti ya biasharanje ya Microsoft.
 • 6. HUDUMA ZA USAIDIZI. Wasiliana na mchapishaji wa programu ili kubainisha huduma za usaidizi zinazopatikana. Microsoft, mtengenezaji wako wa maunzi na mtoa huduma ya pasiwaya (isipokuwa mmoja wao awe ni mchapishaji wa programu) hawawajibiki kutoa huduma za usaidizi kwa programu.
 • 7. MAKUBALIANO YOTE. Makubaliano haya, sera yoyote husika ya faragha, masharti yoyote ya ziada ambayo yanaambatana na programu, na masharti ya vifaa vya ziada na visasisho ndio makubaliano yote ya leseni kati yako na mchapishaji wa programu kwa programu hiyo.
 • 8. SHERIA HUSIKA.
  • a. Marekani na Kanada. Ikiwa ulipata programu nchini Marekani au Kanada, sheria za jimbo au mkoa unaoishi (au, ikiwa ni biashara, mahali eneo lako msingi la biashara lipo) husimamia tafsiri ya makubaliano haya na hutumika kwa madai ya kuyakiuka, na madai mengine yote (pamoja na kuwalinda watumiaji, ushindani usio wa haki, na madai ya makosa ya daawa) haijalishi mgongano wa kanuni za kisheria.
  • b. Nje ya Marekani na Kanada. Ikiwa ulipata programu katika nchi nyingine yoyote, sheria ya nchi hiyo hutumika.
 • 9. ATHARI YA KISHERIA. Makubaliano haya hufafanua haki nyingine za kisheria. Huenda ukawa na haki nyingine chini ya sheria ya jimbo au nchi yako. Makubaliano haya hayabadilishi haki zako chini ya sheria za jimbo au nchi yako ikiwa sheria za jimbo au nchi yako haziruhusu ufanye hivyo.
 • 10. KANUSHO LA WARANTI. Programu imetolewa leseni "kama ilivyo", "na dosari zote" na "kama inavyopatikana". Ni juu yako kuitumia. Mchapishaji wa programu, kwa niaba yake, Microsoft (ikiwa Microsoft sio mchapishaji wa programu), watoa huduma ya pasiwaya ambayo ndio mtandao ambao programu imetolewa, na kila mmoja wa makampuni yetu tanzu, wachuuzi, mawakala na watoa huduma ("Wahusika Walioshughulikiwa"), hawatoi waranti, hakikisho, au masharti kuhusiana na programu. Hatari yote kuhusu ubora, usalama, starehe, na utendakazi wa programu uko juu yako. Iwapo programu itakuwa na kasoro, utagharimia gharama yote ya kuihudumia au kuikarabati. Huenda ukawa na haki za ziada za watumiaji chini ya sheria za nchi yako ambazo makubaliano haya hayawezi kubadilisha. Kwa kiasi kinachoruhusiwa chini ya sheria ya nchi yako, wahusika waliotajwa hawahusishi waranti au masharti yoyote yaliyonukuliwa, ikiwa ni pamoja na uhakikisho wa uuzaji, ubora wa kufaa lengo fulani, usalama, starehe na kutokukiuka.
 • 11. VIZUIZI KUHUSU NA KUTENGWA KWA MAPATANO NA FIDIA. Kwa umbali usiokatazwa na sheria, ikiwa una msingi wowote wa kufidiwa hasara, unaweza kurejeshewa na mchapishaji wa programu hasara zozote za moja kwa moja hadi kiwango ulicholipa kwa programu hiyo au USD$1.00, yoyote ambayo ni kubwa. Unakubali kutofidiwa kwa hasara zozote, ikiwa ni pamoja na zinazotokana na, faida zilizopotea, maalum, isiyo ya moja kwa moja au hasara ya bahati mbaya kutoka kwa mchapishaji wa programu hiyo. Ikiwa sheria ya eneo lako inatekeleza waranti, hakikisho au hali hata kama masharti haya hayafanyi hivyo, muda wake umezuiwa kwa siku 90 kuanzia ulipopakua programu.

Kizuizi hiki kinatumika kwa:

 • Kitu chochote kinachohusiana na programu au huduma zilizopatikana kupitia programu; na
 • Madai ya ukiukaji wa mkataba, waranti, hakikisho, au hali; dhima kali; utelekezaji; au makosa mengine ya daawa; ukiukaji wa sheria au majukumu; au utajiri usio wa haki; au chini ya nadharia yoyote ile; zote kwa umbali unaokubaliwa na sheria husika.

Hutumia pia hata kama:

 • Suluhisho hili halikufidii kabisa kwa hasara zozote; au
 • Mchapishaji wa programu alifahamu au alipaswa kujua kuhusu uwezekano wa hasara.
Maandishi kamili
Huduma ZinazoshughulikiwaHuduma Zinazoshughulikiwaserviceslist
Muhtasari

Bidhaa, programu na huduma zifuatazo zimeshughulikiwa na Makubaliano ya Huduma za Microsoft, lakini huenda zisipatikane katika soko lako.

 • Account.microsoft.com
 • Advertising.microsoft.com
 • Afya na Mazoezi ya MSN
 • Akaunti ya Microsoft
 • Barua ya Windows Live
 • Bing
 • Bing App for Android
 • Bing Bots
 • Bing Business Bot
 • Bing Darasani
 • Bing for Business
 • Bing Image and News (iOS)
 • Bing Search APIs/SDKs
 • Bing Sportscaster
 • Bing Translator
 • Bing Webmaster
 • Bing.com
 • Bingplaces.com
 • Citizen Next
 • Cortana
 • Cortana skills by Microsoft
 • Default Homepage and New Tab Page on Microsoft Edge
 • Dev Center App
 • Dictate
 • Docs.com
 • Duka
 • Duka la Office
 • Duka la Windows
 • education.minecraft.net
 • Eneokazi la Bing
 • Face Swap
 • Familia ya Microsoft
 • Feedback Intake Tool for Azure Maps (aka “Azure Maps Feedback”)
 • Filamu na Televisheni ya Microsoft
 • Forms.microsoft.com
 • forzamotorsport.net
 • Ghala la Picha la Windows
 • Groove
 • Groove Music Pass
 • GroupMe
 • Habari za MSN
 • Hali ya Hewa ya MSN
 • HealthVault
 • Kamusi ya Bing
 • Kisaidizi cha Auni na Urejesho cha Microsoft Office 365
 • Kivinjari cha Wikipedia ya Bing
 • LineBack
 • Michezo ya MSN
 • Michezo, programu na tovuti za Windows zilizochapishwa na Microsoft
 • Michezo, programu na tovuti za Xbox Game Studios
 • Microsoft Academic
 • Microsoft Add-Ins for Skype
 • Microsoft Bots
 • Microsoft Educator Community
 • Microsoft Health
 • Microsoft Pay
 • Microsoft Research Interactive Science
 • Microsoft Research Open Data
 • Microsoft Soundscape
 • Microsoft Translator
 • Microsoft XiaoIce
 • Mixer
 • Msimamizi wa Skype
 • MSN Explorer
 • MSN Premium
 • MSN.com
 • Muziki wa Xbox
 • Mwandishi wa Windows Live
 • Office 365 Binafsi
 • Office 365 Nyumbani
 • Office 365 ya Chuo Kikuu
 • Office Mtandaoni
 • Office Sway
 • Office.com
 • OneDrive
 • OneDrive.com
 • OneNote.com
 • Outlook.com
 • Paint 3D
 • Pasi ya Muziki wa Xbox
 • Pazia ya Microsoft
 • Pesa za MSN
 • Presentation Translator
 • Programu ya Afya ya Kifaa
 • Programu ya Ramani
 • Programu ya Utafutaji ya Bing
 • Programu za Bing
 • Ramani za Bing
 • Remix 3D
 • Rinna
 • rise4fun
 • Ruuh
 • Seeing AI
 • Send
 • Skrini Ifuatayo ya Kufunga
 • Skrini Maridadi ya Kufunga
 • Skype
 • Skype in the Classroom
 • Skype Interviews
 • Skype Qik
 • Skype.com
 • Snip Insights
 • Spreadsheet Keyboard
 • Sprinkles
 • Sway.com
 • to-do.microsoft.com
 • Translator for Microsoft Edge
 • Translator Live
 • Upauzana wa Bing
 • Upigaji Simu wa MSN
 • UrWeather
 • Usafiri wa MSN
 • Utafutaji Maizi
 • Video Breakdown
 • Visio Online
 • Vyakula na Vinywaji vya MSN
 • Watumiaji wa Office 365
 • Web Translator
 • Who’s In
 • Windows Movie Maker
 • Xbox Game Pass
 • Xbox Live
 • Xbox Live Gold
 • Xbox Store
Maandishi kamili
Tarehe 1 Machi, 20180