Trace Id is missing

Kipeto Lugha cha Kiolesura cha Windows 8.1 (LIP)

Kipeto Lugha cha Kiolesura cha Windows 8.1 (LIP) hutoa toleo lililofasiriwa nusu la Kiolesura cha Mtumiaji cha maeneo yanayotumika sana ya Windows 8.1.

Muhimu! Kuchagua lugha hapa chini kutabadilisha maudhui kamili ya ukurasa kuwa lugha hiyo.

  • Toleo:

    1.0

    Tarehe Iliyochapishwa:

    12/11/2013

    Jina la Faili:

    LIP_sw-KE-32bit.mlc

    LIP_sw-KE-64bit.mlc

    Ukubwa wa Faili:

    2.7 MB

    4.1 MB

    Kipeto Lugha hiki Kiolesura cha Windows (LIP) hutoa toleo lililofasiriwa nusu la maeneo yanayotumika sana ya Windows. Baada ya kusakinisha LIP, matini katika vigagula, vikasha ongezi, menyu, na mada za Msaada na auni zitaangazishwa katika lugha ya LIP. Matini ambayo hayajatafsiriwa yatategemea lugha ya Windows 8.1. Kwa mfano, kama ulinunua toleo la Kihispania wa Windows 8.1, na LIP iliyosakinishwa ya Kikatalani, matini mengine yataonekana katika Kihispania. Unaweza kusanidi zaidi ya LIP moja kwa lugha moja msingi. LIPs za Windows zinaweza kusanidiwa kwa matoleo yote ya Windows 8.1.
  • Mifumo ya Uendeshaji Inayotumika

    Windows 8.1

    • Kwa Mahitaji ya Mfumo, bofya hapa

    • Kwa Maagizo ya Usakinishaji wa Mapema, bofya hapa

    1. Bofya kitufe cha Upakuaji kwenye ukurasa huu ili kuanza kupakua, au chagua lugha tofauti kutoka kwa orodha kunjuzi.
    2. Fanya moja ya yafuatayo:
      • Kuanza usakinishaji mara moja, bofya Endesha.
      • Kuhifadhi upakuaji kwenye kompyuta yako kwa usakinishaji wa baadaye, bofya Hifadhi
    • Kwa Maagizo ya Baada ya Usakinishaji, bofya hapa

    • Kwa Masuala Yanayojulikana, bofya hapa