This is the Trace Id: 62f2c182d5ed4547516c2a4fb40fbaeb

Muhtasari wa Mabadiliko ya Makubaliano ya Huduma za Microsoft – Septemba 30, 2025

Tunasasisha Makubaliano ya Huduma za Microsoft, ambayo yanatumika kwenye bidhaa na huduma za mtandaoni za wateja wa Microsoft. Ukurasa huu unatoa baadhi ya muhtasari wa mabadiliko yanayoonekana zaidi katika Makubaliano ya Huduma za Microsoft.

Ili uone mabadiliko yote, tafadhali soma Makubaliano kamili ya Huduma za Microsoft hapa.

  1. Katika kijajuu, tumesasisha tarehe ya chapisho kuwa tarehe 30 Julai, 2025, na tarehe ya kuanza kutumika kuwa tarehe 30 Septemba, 2025.
  2. Katika sehemu ya "Maudhui Yako", tuliongeza sehemu mpya "c." kushughulikia data inayoweza kuhamishwa.
  3. Katika sehemu ya 'Usaidizi', ndani ya sehemu ya 'Kutumia Huduma na Usaidizi', tulifanya masahihisho kwa kuondoa viungo visivyo sahihi na kufafanua kuwa baadhi ya Huduma zinaweza kutoa usaidizi tofauti au wa ziada, na usaidizi kama huo unaweza kutegemea masharti nje ya Makubaliano ya Huduma za Microsoft.
  4. Tuliondoa sehemu ya "Kwa Watumiaji Wanaoishi Australia" chini ya sehemu ya "Usaidizi" kutokana na mabadiliko ya kanuni za eneo.
  5. Chini ya sehemu ya "Asia au Pasifiki Kusini, isipokuwa kama nchi yako imeitwa hapa chini", ndani ya "Huluki Inayotoa Mkataba, Chaguo la Sheria, na Eneo la Kutatua Mizozo", masharti ya wakazi wa Australia yameondolewa kwa sababu ya mabadiliko katika kanuni za eneo.
  6. Katika sehemu ya "Matoleo ya Muda wa Majaribio", ndani ya sehemu ya "Masharti ya Malipo", tuliongeza maneno yanayofafanua kuwa baadhi ya matoleo ya kipindi cha majaribio yanaweza kuhitaji usasishaji kiotomatiki kuwashwa.
  7. Katika sehemu ya "Masharti Maalum ya Huduma", tuliongezea na kufanya mabadiliko yafuatayo:
    • Katika sehemu ya "Huduma za Xbox", ndani ya sehemu ya "Xbox", tulifafanua kuwa kuingia kwenye kifaa au jukwaa ukitumia akaunti yako ya Microsoft, au kuunganisha akaunti yako ya Microsoft kwenye kifaa au jukwaa kama hilo ili kufikia huduma isiyo ya Microsoft, hukufanya usimamiwe na haki za matumizi ya Microsoft yaliyofafanuwa katika sehemu hiyo. Zaidi ya hayo, tulifafanua kuwa mipangilio mahususi ya Xbox ya Usalama wa Familia inaweza kutowezeshwa wakati wa kufikia michezo au huduma za Xbox Game Studios kupitia kifaa au jukwaa la wahusika wengine.
    • Sambamba na mabadiliko yaliyofanywa katika sehemu ya 'Huduma za Xbox', tuliongeza ufafanuzi kwenye sehemu ya 'Vipengele vya Familia ya Microsoft', chini ya sehemu ya 'Xbox', kuhusu mipangilio mahususi ya Xbox ya Usalama wa Familia isiyo na uwezo wa kuwezeshwa wakati wa kufikia michezo au huduma za Xbox Game Studios kupitia vifaa au majukwaa ya wahusika wengine.
    • Marekebisho yalifanywa kwenye sehemu ya "Skype, Microsoft Teams, na GroupMe" ili kuwajibika kwa ajili ya kustaafu kwa Skype.
    • Sehemu ya "Vikwazo na Vizuizi kwenye Pointi", chini ya sehemu ya "Microsoft Rewards", ilirekebishwa ili kuonyesha kwamba muda wa pointi ambazo hazijatumiwa huisha ikiwa hakuna pointi zitakazopatikana au kutumika kwa miezi 12 mfululizo.
    • Sehemu ya "Kughairi Akaunti Yako ya Zawadi", chini ya sehemu ya "Microsoft Rewards", ilirekebishwa ili kuonyesha kwamba Akaunti ya Zawadi inaweza kughairiwa ikiwa hutaingia kwa miezi 12 mfululizo.
    • Sehemu mpya ya vizuizi vya matumizi iliongezwa kwenye sehemu ya "Huduna za Ujasusi Bandia".
    • Sehemu mpya ya "Huduma za Mawasiliano" imeongezwa, ikibainisha kuwa huduma zinazowezesha mawasiliano kati ya watu binafsi, kama vile Skype, Teams, na Outlook, zinategemea masharti ya matumizi ya ziada. Masharti haya yanarejelewa na kuunganishwa ndani ya sehemu hii.
  8. Katika Masharti yote, tumefanya mabadiliko ili kuboresha ufafanuzi na kushughulikia sarufi, uandishi, na matatizo mengine kama hayo. Tumesasisha pia kupeana majina na viungo vya wavuti.